Na Mwandishi wa Brotherdanny5.blog, Arusha
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida madiwani 23 kutokaa katika Halmashauri ya Meru mkoa wa Arusha wametishia kujiuzu wote katika nyadhifa zao lakini pia kukusanya kadi zote za chama cha mapinduzi sanjari na kuongoza maelfu ya wananchi kwenda kuchukua ardhi yao ambayo imetekwa kinyemela,endapo kama Halmashauri hiyo haitatoa tamko rasmi dhidi ya migogoro ya mashamba inayoendelea Wilayani Humo.
Aidha pia kadi ambazo zitakusanywa zitaweza kuwekwa chini ya uangalizi maalumu ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na kazi yoyote ile ya chama cha mapinduzi ikiwa ni fundisho kwa serikali dhidi ya vigogo wake wa Wizara ya Ardhi ambao wanatumika katika migogoro ya ardhi katika Halmashauri Mbalimbali.
Madiwani hao waliyasema hayo ijumaa iliyopita katika baraza la madiwani lililofanyika katika Halmashauri hiyo ambapo agenda ya migogoro ya ardhi ilifanya baraza hilo kujikuta likiwa linatoa tamko na vitisho vikubwa kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.
Akiongea kwa niaba ya madiwani wa Halmashauri hiyo bi Mwanaidi Kimu alisema kuwa wameschoshwa kila siku kujadili agenda za migogoro ya ardhi lakini hakuna utendaji wowte na badala yake wanabaki wakiwa na kumbukumbnu ya vikao katika vichwa vyao hali ambayo kwa sasa imefika mwisho
Akitolea mfano moja yashamba lenye migogoro katika Halmashauri hiyo,shamba la Madira lililopo katika maeneo ya Seela Singisi ambalo ni mali halisi ya Halmasahuri hiyo lakini kwa sasa kuna migogoro ambayo inasababishwa na baadhi ya viongozi jambo ambalo wamedai kuwa hawataweza kuvumilia bali wataingia katika vita kwa mara nyingine
“Kwa mfano hili shamba la Seela Singisi ni mali ya wananchi wote wa Meru na hadi Raisi ameshaweka saini yake jamani litumike kwa ajili ya matumizi ya kata zote za Meru lakini vigogo wanasema ni mali yao alafu bado tumenyamaza tu haitawezekana tunaachia udiwani alafu htunaingia katika Vita kwa mara nyingine”aliongeza Kimu
Katika hatua nyingine akiongea kwa niaba ya madiwani wanaume ,Wilson Nyitti alisema kuwa hali hiyo imesababisha kila wanpopita walazimke kujikuta wakiwa wanazomewa ovyo na wananchi kwa kuwa wananchi wanafikiri kuwa wao wananufaika na migogoro hiyo ya ardhi
Nyitti alisema wamechoka na hali hiyo ya kudhomewa na kuabishwa mara kwa mara wakati hawausiki na kutokana na hilo sasa wamejipanga kushirikiana na wananchi kurudi kwanye vita kwa mara nyingine kwa ajili ya kuchukua ardhi yao lakini kupigana hata ikiwezekana kabisa.
“hili ni tamko rasmi tunatoa tunataka majibu ya migogoro hii rasmi kama hatupewi itakuwa ni vita baina ya Wameru na hawa wanaojichukulia ardhi kinyemelea, pia itakuwa ni huzuni kubwa kwa CCM manake kwanza sisi wote hapa tunatokea CCM uzalendo umetushinda kabisa”aliongeza Nyiti
Naye Mwenyekiti wa Halmasahuri hiyo ya Meru, Goodson Majola alisema kuwa tamko hilo la kutaka kujiuzulu kwa madiwani 23 wote wa halmashauri hiyo lipo sawa kabisa kwa kuwa migogoro yote ya ardhi inasababishwa na Viongozi wasio waadilifu kuanzia ngazi ya Halmashauri hadi Wizara
Akiongelea suala la shamba hilo la Madira alisema kuwa Raisi Kikwete tayari ameshatoa ardhi hiyo yenye jumla ya Hekari 360 lakini bado hawajaweza kulitumia kutokana na vitisho ambavyo walikuwa wanavipata kutoka kwa vigogo
“Mimi nasema kuwa tutajiuzulu wiki chache zinazokuja baada ya kujiridhisha juu ya maangaiko haya ya ardhi ambayo yamedumu toka karne hadi karne na ninasiistiza kuwa itakuwa ni kilio kwa CCM kwa kuwa wanchama wetu nao tutaweka chini ya ulinzi hadi tutakapowaambia hawatajishugulisha na shuguli yoyote ya chama,” alisema Majola.
Majola alisema kuwa kujiuzulu kwao lakini pia kuondoka na wanachama wote wa CCM katika Wilaya hiyo ni uzalendo wao kwa wananchi na hivyo Hata CCM nao hawapaswi kuumia kwa hilo.
Hata hivyo, halmashauri hiyo inaoongozwa na madiwani wote wa CCM lakini pia kwa upande wa wapinzani inaongozwa na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari.
No comments:
Post a Comment