Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akiandika huku akitafakari jambo wakati wa uzinduzi huo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe akielezea umuhimu wa wananchi kupima virusi vya ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B).
Meza kuu wakibadilishana mawazo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akizindua rasmi kampeni ya kupambana na ugonjwa hatari wa Homa ya Ini.
Ini likiwa salama kabla ya kushambuliwa na virusi vya Hepatitis B.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick amezindua rasmi kampeni ya kupambana na Ugonjwa wa Homa ya Ini katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam.
Kampeni hiyo imeandaliwa na Kampuni ya Global Pulishers Ltd wakishirikiana na Wizara ya Afya, SD Africa, Sanofi, Megra Clinic, Damu Salama na Tamsa.
Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewataka wadau mbalimbali kuonyesha ushirikiano katika kupambana na ugonjwa huo hatari kuliko HIV huku akiwaasa wananchi kuacha vitendo vinavyoweza kuleta maambukizi ya ugonjwa huo unaombukizwa kwa njia sawa na za HIV.
(PICHA ZOTE NA GPL)
No comments:
Post a Comment