Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 3 January 2015

PANYA ROAD WATINGISHA DAR, WAFANYA UPORAJI, WANANCHI WAKIMBIA OVYO

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova 
Na Waandishi Wetu, Mwananchi
Dar es Salaam. Kwa mara nyingine tena, taharuki, hofu na wasiwasi mkubwa viliwakumba wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa saa mbili baada ya kundi maarufu la waporaji la Panya Road, kuvamia mitaa mbalimbali na kupora mali.
Taarifa za kundi hilo lililopora watu katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo zilienea kwa kasi ya ajabu kupitia mitandao ya kijamii watsap, twitter, jamii forum, blog, instagram na ujumbe mfupi wa simu.
Baada ya maeneo ambako kundi hilo linadiwa kufanya uporaji ni Tabata, Magomeni Kagera, Sinza, Mwananyamala, Kinondoni, Kijitonyama, Manzese, Kigogo na Buguruni, huku wanafunzi wanaoishi katika Hosteli za Chuo Kikuu Dar es Salaam, wakitoka nje ya mabweni yao kwa kuhofia kuvamiwa na kikundi hicho.
Taharuki hiyo iliyoanza saa mbili usiku, ilisababisha wakazi wa maeneo mengi ya jiji kujifungia ndani, huku wafanyabiashara wakifunga maduka na kujificha wakihofia kundi hilo la wahalifu.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment