Bill Gates na Warren Buffet
Huku wafanyibiashara na wanasiasa wa ngazi za juu wakikutana katika mkutano wa kiuchumi duniani mjini Davos wiki hii ,hisia tofauti zimetolewa kuhusiana na kuwepo kwa ukosefu wa usawa duniani bila kuisahau asilimia moja ya watu Matajiri duniani.
Matajiri hao wanaishi katika visiwa vya kibinafsi, lakini je, hao ndio matajiri wanaojulikana pekee?
Ripoti moja ya Shirika la Wahisani la Oxfam iliyotolewa sanjari na mkutano huo wa Davos, ilizua hisia kali baada ya kubashiri kwamba asilimia moja ya matajiri duniani huenda ikamiliki idadi yote ya watu duniani.
Ilitoa utafiti wake kutoka kwa benki ya Credit nchini Uswizi ambayo inakadiria jumla ya utajiri katika kila nyumba kuwa dola trilioni 263.
Huo ni utajiri na wala si mapato.
Watu matajiri kama vile Bill Gates, Warren Buffet na Mark Zuckerberg ni miongoni mwa asilimia 1.
Lakini je, ni nani mwengine aliyeorodheshwa katika asilimia hiyo?.
Kulingana na ripoti hiyo ya benki ya Credit watu wengine millioni 47 wana utajiri wa dola 798,000 kila mmoja.
Hiyo inashirikisha watu wengi katika mataifa tajiri ambao pengine wasingejitambulisha kama matajiri,lakini ambao wanamiliki nyumba ama wamelipa kiwango kikubwa cha mkopo.
Miongoni mwao ni:
Watu milioini 18 wanatoka Marekani
Milioni 4 wanatoka Japan
Watu milioni 3.5 wanatoka Ufaransa
Watu milioni 2.9 wanatoka Uingereza
Milioni 2.8 wanatoka Ujerumani
Na milioni 1.6 wanatoka China
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment