Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 13 January 2015

WAONYWA KUTOINGIZA SIASA KWENYE MIRADI


Na Hastin Liumba, IgungaSERIKALI Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora imeonya na kuwawataka wana siasa  kuondoa tofauti zao za kisiasa katika kutekeleza na kusimamia mfuko wa Tasaf awamu ya Tatu.

Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Alphonce Kasanyi  alisema hayo wakati akifungua walsha hiyo ya kuwajengea uelewa viongozi na watendaji katika Halmashauri ya wilaya ya Igunga. 
Alisema kuwa baadhi ya wanansiasa hutumia miradi ya kitaifa kuidhorotesha na kuingiza kuacha siasa katika na malengo ya mradi husika.
Alisema kuwa Tasaf awamu ya Tatu inalengo la kuzibaini kaya masikini na kuzinuru kupitia mipango yake madhubuti iliyopangwa bila kujali itikadi za kisiasa,Dini na kikabila.
Alisema kuwa wananchi wanapaswa kuelewa madhumuni ya Tasaf kwa jamii na kuwataka kuwapuuza wanasiasa watakao tumia mwanya huo kupenyeza maneno yao tofauti na malengo husika.
Aliwataka wanasisas kuwa kitu kimoja katika kuhamasisha wnanchi dhidi ya Tasaf na kuondoa tofauti zao huku wakisimamia kikamilifu mpango huo ambao unalenga kunusuru kaya masikini. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Igunga  Abubaakari  Shaabani aliwataka wawezeshaji wamradi huo kutenda haki kwa kubaini kaya masikini kwani kuna baadhi wanaweza kufanya upendeleo.
 Aliiomba serikali pale patakapo tokea uchakachuaji wa kaya masikini hatua kari za kinidhamu zishike hatua ilikuhakikisha haki inatendeka mara moja.

No comments:

Post a Comment