Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati meza-kuu) akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na Serikali kuunda timu maalumu ya kutembelea
maeneo yaliyosugu kwa utekaji na mauaji ya albino nchini ambapo timu hiyo
inatarajiwa kuanza kazi wiki mbili zijazo kwa kuanza na mikoa sugu ya matukio
hayo ambayo ni Mwanza, Geita, Simiyu, Tabora na Shinyanga na baadaye itafuata
mikoa mingine. Pia Waziri Chikawe katika mkutano huo, alitangaza kupiga
marufuku wapiga ramli wote nchini kwa kuwa wanasababisha kuendelea kwa matukio
ya kinyama wanayotendewa albino. Hata hivyo, katika mapambano ya kusambaratisha
unyanyasaji huo, waziri huyo alitangaza kushirikiana ipasavyo na viongozi wa
dini pamoja na mashirika ya kijamii ili kusaidia kutoa elimu kwa wananchi kutokana
na uhalifu huo dhidi ya albino. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, IGP Ernest Mangu na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini
(TAS), Ernest Kimaya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa
wizara hiyo, jijini Dar es Salaam juzi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati meza-kuu) akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na Serikali kuunda timu maalumu ya kutembelea
maeneo yaliyosugu kwa utekaji na mauaji ya albino nchini ambapo timu hiyo
inatarajiwa kuanza kazi wiki mbili zijazo kwa kuanza na mikoa sugu ya matukio
hayo ambayo ni Mwanza, Geita, Simiyu, Tabora na Shinyanga na baadaye itafuata
mikoa mingine. Pia Waziri Chikawe katika mkutano huo, alitangaza kupiga
marufuku wapiga ramli wote nchini kwa kuwa wanasababisha kuendelea kwa matukio
ya kinyama wanayotendewa albino. Hata hivyo, katika mapambano ya kusambaratisha
unyanyasaji huo, waziri huyo alitangaza kushirikiana ipasavyo na viongozi wa
dini pamoja na mashirika ya kijamii ili kusaidia kutoa elimu kwa wananchi
kutokana na uhalifu huo dhidi ya albino. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini, IGP Ernest Mangu na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Albino
nchini (TAS), Ernest Kimaya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano
wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam juzi. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA
MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment