Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 26 January 2015

WATANZANIA WALILIA TAIFA HURU


Na Hastin Liumba, TaboraWAKATI Taifa likikiwa limetimiza  miaka 54 tangu lipate uhuru wake kutoka kwa wakoloni sasa watanzania waanza kulilia uhuru Mpya kutokana na Udhalimu unaolikabilii taifa hili kwa sasa.


Kauli hiyo imetolewa  na Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Masendeleo {CHADEMA} Mkoani Tabora katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya mabasi ya zamani wakati wakiwaaga Vijana waliotembea kilometa 1400 kwa Miguu kutoka Mkoani Geita kwenda Jijijini Dar es Salaam.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Viongozi hao wa Chadema walisema Vijana hao ambao ni watatu ni miongoni mwa Vijana 200 wa Mkoa wa Geita waliokuwa wanaenda kumweleza Rais  wa Jamhuri Ya Muungano Tanzania Dk.Jakaya Kikwete jinsi wananchi wanavyoteseka nchini kwao.

Walisema vijana hao walikuwa na mambo matatu ya kumweleza Rais ambayo Watanzania wnatamani yafanyike ili kulinusuru taifa la Tanzania lilojaa Ufisadi, Unyanyapaa,Uonevu,Ujangiri,na udhalimu na hata ubaguzi wa rangi.

Aidha mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Tabora Francis Msuka alisema vijana walitaka kumwambia Rais Kikwete kuwa watanzania wanahunishwa na ufisadi wa Viongozi walioko madarakani na  uhujuma wa rasilimali za watanzania ,Mauji ya wananchi wasikuwa na hatia yanayozidi kufanyika kila kukicha ikiwa ni pamoja kudai Taifa Huru kama livyokuwa mwaka 1961.

Alisema wananchi kwa sasa hawadhaminiki wala hawaonekani kama wanaumuhimu ndaini ya lao kutoka na Vingozi walioshika dora kuweka masrahi yao mbele badala ya maendeleo ya Nchi.

Msuka alisema  Serikali imejaa Wezi wengi bila kujua kuwa ni Dhambi kuhujumu Taifa na Kuliacha hali masikini huku wanachi Masikini wakipelekwa Kufungwa na wengine kuchomwa Moto kama wezi na kusahau kuwachoma Moto wanaohujumu fedha za Serikali.

“Na kama adhabu ya Mwizi ni Kupigwa mawe hadi kufa ikiwa ni pamoja na kuchomwa moto je waliohusika na ukwapuaji wa Escrow wako wapi kwa sasa adhabu hiyo imesubiliwa nini kuchukuliwa dhidi yao”alihoji Mwenyekiti.

Kwa upande wake Mmoja wa Vijana hao waliotembea Kilometa 1400 alisema Laiti kama askali Polisi nao wangetambua haki yao wangeungana na wanacnhi wanyonge kudai Taifa huru lenye kuzingatia misingi ya haki
kwa kila mtu.

Alisema msingi ya haki Imevurugwa na sasa wnanachi watanzania wamebaki hali masikini huku wakikosa mtu wa kuwasaidia ambapo amewataka  wakazi wa Mkoa wa Tabora kufumbua macho na kutambua wajibu wao ndani ya taifa lao.

Alieleza kuwa Nchi imejaa unafiki na ukitaka kujua alama za mtu Mnafiki ni kuongea uongo na kupotosha umma,kutotimiza ahadi pindi anapoahidi ikiwa ni pamoja na akithaminiwa na kuaminiwa hasau fadhila za aliyemwani na badala yake hujinufaisha mwenyewe.

Hata hivyo alisema kuwa vyombo vya dora vimewekwa kwa ajili ya watu masikini tu kwani ukiangalia watu wengi wanaotumikia jera ni watoto wa maskini tu hali Vigogo wanaohujumu nchi wakizidi kupeta pasipo kutiwa hatiani.

No comments:

Post a Comment