Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 13 January 2015

MVUA ZA MASIKA ZALETA MAAFA NZEGA

Na Hastin Liumba, NzegaWATU watatu katika matukio mawili tofauti wamefariki dunia katika Kijiji cha Ugembe wilayani Nzega mkoani Tabora kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha.

Akizungumza na waandishi wa habari Diwani wa Kata ya Mwakashanhala Julius Mshandete alisema kuwa tukio la kwanza mtoto mwenye umri wa miaka minne amefariki dunia baada ya kutumbukia kisimani wakati akicheza na wenzake.
Alimtaja mtoto huyo kuwa ni Nkamba Dalali ambaye alidumbukia katika kisima kilichokuwa kimejaa maji kutokana na mvua kubwa iliyoyensha Januari 11, mwaka huu.
Katika tukio la pili watu wawili wamefariki dunia baada ya kudondokewa na ukuta wa nyumba waliyokuwa wamelala usiku wa kuamkia Januari 11, mwaka huu baada ya mvua kubwa kunyesha huku watu watano wakijeruhiwa na ukuta huo tukio hilo limetokea katika kijiji cha Ugembe kata mpya ya ugembe majira ya saa kumi alfajiri.
Alisema kuwa majeruhi hao hawajapelekwa hospitali kutokana na miundombinu ya barabara kuhariba na kuongeza kuwa hali zao zinaendelea vizuri kutokana na kutoumia sana miili yao.
Diwani  Mshandete aliwataja watu hao walifariki dunia kwa kudondokewa na ukuta kuwa ni pamoja na Nyamate Shija (70) na Luja Marco (15) wote wakiwa wakazi wa kijiji hicho.
Alisema kuwa matukio hayo yakusikitisha yamesababishwa na mvua za masika zinazoendelea kunyesha na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kuwa waangarifu na nyumba zinazoonesha dalili mbaya za kudondoka ilikunusuru maisha yao na kuepusha ulemavu.
Aliwataka wazazi na walezi kuwa waangalifu kwa watoto kutokana na madimbwi na mabwawa pamoja na visima kujaa maji ilikuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Kamanda wa polisi mkoani Tabora Kamishna msaidizi (ACP) Suzan Kaganda amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na upelelezi unaendelea  ilikubani sababu kuu na kuwataka wananchi kuwa waangalifu katika kipindi hiki cha mvua za masika.

No comments:

Post a Comment