Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Tuesday 13 January 2015
WAKULIMA BINAFSI WA TUMBAKU WAONYWA
Na Hastin Liumba,TaboraCHAMA kikuu cha wakulima wa zao la tumbaku kanda ya magharibi (WETCU) kimefanya mkutano wa uchaguzi wa wajumbe wa bodi ambapo Mkandala Gabriel Mkandala amechaguliwa kuwa mwenekiti mpya kwa kura 401.
Katika uchaguzi huo Mkandala alishinda nafasi hiyo kwa kura 401 za ndiyo kati ya 418 zilizopigwa huku 16 zikiwa za hapana na moja ikiharibika kwani hakuwa na mpinzani.
Uchaguzi huo umefanyika chini ya uenyekiti wa Mossi Chongelo kaimu mrajisi wa vyama vya ushirika nchini kunafuatia kusimamishwa kwa bodi iliyokuwepo kuondolewa mwezi marchi 2013 kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali za chama.
Nafasi ya makamu mwenyekiti imechukuliwa na Msafiri Ngassa kwa kura 253 akiwabwaga wapinzani wake Abel Willison aliyepata kura 131 huku Rajab Hamis akiambulia kura 51 kati ya zilizopigwa 426.
Wengine waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa bodi ni Kabansi Mayagillo, Rajab Hamis, Abel Willison, Athanas Vallentino, Izaki Jakobo na Phillipo Pascal huku nafasi moja ya mjumbe kutoka Urambo ikibaki wazi kwa vile kati ya walioomba hakupatikana aliyekidhi vigezo vya kugombea.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo mwenyekiti mpya amewaonya wakulima wa kujitegemea na kuahidi kuwachukulia hatua kali wanaojaribu kuua vyama vya msingi vya ushirika.
Mkandala ambaye anashika wadhifa huo kwa miaka mitatu ijayo amesema hatosita kuwachukulia hatua kali za kisheria wakulima wa kujitegemea endapo hawatazingatia sheria ya ushirika inavyosema.
Amewaonya wakulima hao wasijaribu kujihusisha na kuu vyama vya ushirika atakayethubutu kufanya hivyo atapambana naye.
Akizungumza katika mkutano huo kaimu mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Mossi Chongelo ameitaka bodi hiyo mpya itekeleze matakwa ya wanachama kwani wao ndiyo wamekabidhiwa hiyo dhamana.
Hali kadhalika amewashauri wanachama wa vyama hivyo kujiendeleza kielimu ili kuendana na matakwa ya sheria mpya ya ushirika namba 6/2013 ambayo inawataka viongozi kuwa elimu ya zaidi ya kidato cha nne.
Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi Deogratias Ruganyika aliwataka wanaushirika kutoa ushirikiano kwa viongozi hao wapya ili waweze kuwatumikia ipasavyo.
Katika hatua nyingine aliyekuwa mwenyekiti wa muda wa badi hiyo Hassan Wakasuvi alionyesha kukelwa kwake na sheria hiyo mpya ya ushirika hasa katika uombaji nafasi za uongozi.
Wakasuvi alisema kuwa sheria hiyo inawaona ni watu wazuri wakati wa uzalishaji mazao lakini baadaye wanapotaka nafasi za uongozi wanakuwa wabaya pale inapowawekea masharti magumu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment