Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu
Na Hastin Liumba, TaboraJESHI la Polisi mkoani Tabora linamshikiria mama mmoja mkazi wa kata ya Chemchem katika Manispaa ya Tabora Zuhura Masudi 25 kwa kosa la kuwanyonga hadi kufa watoto wake wawili.Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Juma Bwire alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema tukio hilo lilitokea januari 25, mwaka huu majira ya saa moja jioni maeneo ya Chechem katika Manispaa ya Tabora.
Aliwataja marehemu hao kuwa ni Mwamvua Mrisho miaka 4 na mwingine aliyetambulika kwa jina moja la Sudi anayekadiliwa kuwa na umri wa miezi 4.
Alisema kwamba baada ya mama huyo kutekeleza mauaji hayo aliwavilingisha katika mifuko ya sandarusi kisha kuwafukia chini mmoja sebuleni na mwingine chumbani kwake.
Kamanda Bwire alisema tayari mama huyo pamoja na baba yake mzazi aitwaye Shabani Ramadhani miaka 75 wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi, kwakuwa inadaiwa kwamba kulikuwa na ugonvi wa kugombea nyumba kati ya mama huyo na mzee Shabani.
Alisema kuwa jambo hilo labda ndiyo kilikuwa chanzo cha mama huyo kuamua kuchukua maamuzi magumu kama hayo ya kuuwa manawe.
Aidha kamanda Bwire alisema jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi zaidi ili kuweza kubaini chanzo halisi cha kutokea vifo hivyo na kwamba baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa hao wanatafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
No comments:
Post a Comment