Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 16 January 2015

COASTAL UNION WAICHIMBA MKWARA POLISI MORO

Displaying KIKOSI.jpg
Kikosi cha Coastal Union

NA MWANDISHI WETU, TANGATIMU ya Coastal Union imeitahadharisha timu ya Maafande wa Polisi Morogoro kwa kuiambia isitarajie kuwa itaweza kuchukua pointi tatu muhimu wenye kwenye mechi yao ya Ligi kuu itakayochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani badala yake wajiandae kupokea kipigo kutoka kwa timu hiyo kutokana na maandalizi kabambe waliyoyafanya kuelekea mechi hiyo.


Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Jumapili wiki hii ikiwa ni muendelezo wa Michuano ya Ligi hiyo iliyoanza Septemba 26 mwaka jana hapa nchini.

Tambo hizo zilitolewa leo na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mkenya James Nandwa mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini hapa.

Amesema kuwa kikosi cha timu hiyo kimeimarika zaidi kutokana na kufanya marekebisho madogo madogo yaliyojitokeza kwenye mechi yao iliyopita na sasa wapo tiyari kuikabili timu yoyote ile kwenye michuano hiyo.

Amesema tayari safu mbalimbali kwenye timu hiyo zimekwisha kuwa imara jambo ambalo linampa matumaini makubwa kuwa na uhakika wa kubakiza pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo ambao wataingia wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi iliyopita.

    “Kila mechi sisi kwetu sio ya kubeza hivyo tutahakikisha tunapambana kufa na kupona lengo likiwa kuweza kupata matokeo mazuri yatakayoweza kutusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi hiyo “Amesema Kocha Nandwa.

Amesema kuwa timu hiyo imejipanga imara kuweza kufanya vizuri kwenye michezo yake iliyosalia kwenye raundi ya kwanza kwa kuweka mipango mizuri itakayowezesha kufikia malengo hayo.

Akizungumza hali ya majeruhi, Kocha Nandwa amesema kuwa kikubwa anacho mshukuru mungu ni kikosi hicho kutokuwa na majeruhi hata mchezaj mmoja na kuwahaidi wapenzi na wadau wa soka burudani.

No comments:

Post a Comment