Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage
Na Mwandishi Wetu, Tabora
VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Matawi na Kata za Misha na Kabila wamerudisha baiskeli zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail Aden Rage kutokana na madai ya maneno waliyodai ni kashfa kwao na kuona kama wamedhalilishwa na mbunge wao.
Makatibu Kata na wenyeviti wa kata ya Misha na Kabila walikabidhi baiskeli hizo kwa katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tabora Mjini Bakar Luasa walisema kuwa wamechoshwa na kashifa za Mbunge huyo ndiyo sababu ya kurudisha baikeli hizo.
Mbunge huyo amejikuta katika mzozo mkali kwa baadhi ya viongozi wa kata kurudisha baiskeli,alizotoa kwa ajili ya kufanyia kazi za chama kwa kuwatolea maaneno ya kashfa.
Waliorrejesha baiskeli hizo ni katibu kata ya Misha Bonifasi Mkinga,Mwenyekiti wa kata ya Kabila Juma Lukindo Lububu,Katibu wa UVCCM Ramadhani Hassani wa kata ya Kabila, katibu tawi, kata ya Kabila Juma Misayo ,Katibu Tawi John Makoloma wa Kata ya kabila.
Mmoja wa Viongozi hao wa kata ya Misha Bonifasi Mkinga alisema kuwa,Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini,Ismail Aden Rage mara nyingi hukashifu na kuwanyanyasa Viongozi na hata wananchi kwa wale wanao mtolea shida wanapewa lakini baadae wanatangazwa na kudaiwa wana njaa.
Mkinga alisema kuwa mnamo mwezi Mei 19, mwaka 2014 mbunge huyo alitoa baiskeli 18 aina ya Sport ambazo zilikuwa ni mbovu kiasi lakini kikubwa hadi wamerejesha baiskeli hizo ni matusi na kashfa.
Waliongeza kuwa wamekuwa twakipata kashfa nyingi kutoka kwa mbunge huyo,Mnamo Januari 23.mwaka huu majira ya saa 12.30 jioni Ismail Aden Rage alikwenda kijiji cha Masagala kuangalia kisima cha pampu kilichoharibika,ili akitengeneze na alikuwa na mafundi wake wa kufunga pampu.
Bonifasi Mkinga Aliendelea kusema kuwa Siku alipokuja akiwa na mafundi hao alikutana na mimi katika kijiji cha Masagala na kuanza kunishutumu kuwa mimi ni mwizi na tapeli wa fedha alizokuwa akitoa kama mbunge ili apewe katibu kata wa vijana wa Misha.
Bonifasi alisema kuwa ananishutumu kuwa mimi tapeli na nimenunuliwa na mwanachama mmoja,lakini sisi tunamjua kuwa yeye ni Mbunge wetu wa jimbo la Tabora Mjini katika kipindi cha miaka mitano lakini kwanini aseme maneno kama hayo.
Lakini nashangaa sana kuwa yeye anatoa kashifa kuwa anatulipa kila mwezi shilingi Elfu kumi (10,000) na baiskeli amewapatia kwa ajili ya kazi za chama.
Mnamo mwezi Januari 8, 2015 nimerudisha baiskeli yake kwa kutukashifu kuwa sisi matapeli wa fedha zake, tumeona jambo la msingi tumrudishie hizo baiskeli zake," alisema.
Kwa upande wa Katibu wa chama cha mpinduzi CCM Bakali luasa alisema kuwa alipokea baiskeli hizo kutoka kwa makatibu hao na nimewapa siku mbili kutoa maelezo juu ya kurudisha kwa baiskeli walizopewa na mbunge.
Katibu huyo amewataka wanachama kuwa makini katika kipindi hiki kinachokuja cha uchaguzi kuzingatia utaratibu wa chama cha mapinduzi wa mwaka huu wa 2015 vinginevyo watajikuta katika mdomo wa mamba.
No comments:
Post a Comment