Askari jeshi wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa kundi haramu Boko Haram wameteka watu zaidi ya 60 katika nchi jirani ya Cameroon imethibitika.
Inasemekana miongoni mwa mateka wengi wao ni watoto waliokamtwa mpakani mwa nchi mbili hizo.Na inaarifiwa kuwa watu kadhaa waliuawa wakati wa utekelezaji wa tukio hilo.
Boko Haram siku za hivi karibuni zimekamata udhibiti wa miji kadhaa na vijiji upande wa kaskazini Mashariki mwa Nigeria, na sasa wameanza kuwa tishio kwa nchi jirani wanazopakana na Nigeria .Katika shambulio hilo la siku ya Jumapili askari hao walivamia vijiji viwili vilivyoko eneo la Tourou .
Katika uvamizi huo nyumba kadhaa zilichomwa moto na idadi ya mateka ni themanini kati yao watu wazima ni thelathini,na watoto wapatao hamsini na walielekea upande wa Kaskazini mwa Cameroon .
Kundi hilo limepigana vita takribani miaka sita sasa, wakijaribu kuusimika utawala wa dola ya kiislam nchini humo.
Cameroon imekuwa ikiishutumu Nigeria kwa kushindwa kufanya juhudi za ziada za kukabiliana na kundi hilo la Boko Haram.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment