Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akibadilishana hati ya makabidhiano ya vifaa vya michezo na Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing (kulia) wakati wa hafla ya kukabibidhiana vifaa hivyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija)
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabibidhiwa msaada wa vifaa vya michezo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Balozi wa China hapo nchini Lu Youqing na Mwakilishi Mkuu wa Wafanyabiashara kutoka China waishio nchini Lin Zhiyong. Jumla ya vifaa kumi na nne vimetolewa ambavyo ni Roboti ya kujifunzia mpira wa Meza, Kifaa cha kupimia upepo kwa ajili ya Riadha,Nyavu ya mpira wa Meza, Mashine ya kupimia Uzito,Ulingo wa Ngumi, Kompyuta, Printa, Radio Call, mashine ya kutafsiri na kuhesabu matokeo katika riadha na nyaya za umeme vyenye thamani zaidi ya 200.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akicheza Mpira wa Meza na Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing (kulia) wakati wa hafla ya kukabibidhiwa msaada wa vifaa vya michezo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing akielezea namna mmtambo wa Radio Call unavyofanya kazi, katika mwenye blauzi ya kitenge Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara, na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda
Ulingo wa kisasa uliokabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China mwishoni mwa wiki jini Dar es Salaam.
Na
Benjamin Sawe, WHVUM
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo imepokea msaada wa vifaa mbalimbali vya mchezo wa ngumi na riadha
kutoka kwa Serikali ya Watu wa China vyenye jumla ya thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk.
Fennela Mukangara alisema msaada huo ni sehemu ya kuboresha tasnia ya michezo
ikiwa ni pamoja na kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu baina ya nchi hizo
mbili.
“Msaada huu ni kiashirio tosha kwa wananchi wa nchi
zote mbili na umekuwepo ukiendelea kuimarika na tunazo fursa za kuendeleza
ushirikiano huu kwa manufaa ya wananchi wetu”.Alisema Mheshimiwa Mukangara.
Aidha alimuhakikishia Mheshimiwa Balozi wa China
kuwa Watanzania wanathamini mchango mkubwa wenye lengo la kuendeleza michezo
hapa nchini kwani China na Tanzania zina historia ya pamoja ya takribani ya
miaka 50 mpaka sasa.
Alisema kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa imewasilisha kwenye ofisi ya Ubalozi wa China mapendekezo ya kuendeleza
ushirikiano kupitia sekta ya michezo ambapo matumaini yake ni kuwa kwa kupitia
maeneo hayo zitapatikana fursa zaidi kwa vijana kuendeleza ushirikiano
baina ya
nchi mbili kupitia michezo ikiwa ni pamoja na kujifinza mambo muhimu
katika tasnia ya Michezo.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mh. Lu
Youqing alisema Serikali yake itaendelea kuwa na ushirikiano na Serikali ya
Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwa ni ishara ya kudumisha ushirikiano baina
ya nchi hizo mbili.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na “Table Tennis 2”, Wind Speed Gage Device 2,
“UPS 1, Table Tennis Net” 7, “Electronic Weigher 2”, Computer 1, “Table Tennis
Balls”, “Boxing Ring 2”, “Table Tennis 5”, “Printer 1”, “Electronic Cable 6”,
“Radio Call 2”, “Anemograph 2”, na Electric Timing and Scoring Interpretation
Device For Finishing line 1” ambapo jumla yake ni zaidi ya shilingi milioni
200.
Mpaka sasa
Serikali ya China imeshaipatia msaada Serikali ya Tanzania jumla ya shilingi bilioni moja ili
kuendeleza sekta mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment