NA MWANDISHI WETU, TANGA
TIMU ya soka Coastal Union ya Tanga imeitumia salama timu ya Yanga kuwa isitarajie itaweza kuchukua pointi tatu kirahisi kwenye mechi yao itakayochezwa Jumatano wiki hii ya Ligi kuu kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani badala yake ijiande kwa kipigo kutokana na maandalizi walioyafanya kuelekea mchezo huo.
Akizungumza LEO,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa asilimia kubwa ya mapungufu yaliyojitokeza kwenye timu hiyo yamefanyiwa marekebisho na kikosi cha timu hiyo kipo tayari kuweza kuwakabili wana jangwani hao kwa kupata ushindi.
Amesema kuwa katika mechi zake alizocheza amekijua vema kikosi hicho hivyo anaamini dozi ambaye ameanza kutoa kwao itaweza kuwabadilisha vilivyo kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye michezo yao ya ligi kuu soka Tanzania bara.
“Tokea tulipomaliza mechi yetu na JKT Ruvu tumekuwa tukiwapa wachezaji wetu mazoezi ya nguvu kuhakikisha safu mbalimbali zinaimarika kabla ya kuwavaa Yanga, ninaamini tutafanya vema kwa sababu timu zote za Ligi kuu soka Tanzania bara zitahitaji pointi tatu nasi tunahitaji hizo hizo “Amesema Assenga
Akizungumzia hali za wachezaji, Kocha Mkuu wa timu hiyo,James Nandwa amesema wachezaji wote wapo imara kwa ajili ya mchezo huo ambao kwa lengo la kuhakikisha wanapambana vilivyo ili kuweza kubakiza pointi tatu kwenye uwanja wao wa nyumbani mkwakwani.
Coastal Union itaingia kwenye mechi hiyo ikiwa ni kumbukumbu ya kupoteza mechi yao na Jkt Ruvu kwa kufungwa bao 1-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani.
No comments:
Post a Comment