Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 7 January 2015

KITUO YATIMA CHASAIDIWA MAGODORO


Na Hastin Liumba, Igunga
KITUO cha kulelea watoto yatima na walio katika mazingira magumu cha Charity and Orphanage Organization (CAO) cha wilayani Igunga mkoani Tabora kimekabidhiwa msaada wa magodoro matano yenye thamani ya sh.275,000.



Msaada huo wa magodoro umetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani Tabora Seif Hamis Gulamali katika hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo mwishoni mwa wiki.

Akikabidhi msaada huo Gulamali alisema ametoa ili kupunguza changamoto kadhaa zinazokikabili kituo hicho na hasa ikizingatiwa  watoto walioko katika kituo hicho ndio watakaokuwa viongozi wa baadaye.

Alisema hali ya huduma kwa watoto walioko katika kituo hicho chenye takribani watoto 15 hairidhishi hususani katika suala zima la malazi kwani wanalala katika vitanda visivyo na matandiko ya godoro.

Alisema kuongezeka kwa watoto wa mitaani kunachangiwa na hali ya umasikini inayowakabili wazazi na walezi walio wengi ambao aidha hushindwa kumudu mahitaji yao ya kila siku kutokana na ugumu wa maisha.

Gulamali aliongeza kuwa ipo haja ya jamii kuendelea kujitoa kwa kuwasaidia watoto na wanajamii wengine wenye mahitaji kwani bila jamii kujitoa kusadiana idadi ya watoto wasiojiweza na yatima itaendelea kuongezeka mitaani hali ambayo itafanya ongezeko hilo kuwa kubwa na hivyo kuwa janga la taifa.

Aidha alisema serikali ikiweka misingi bora au utaratibu unaoeleweka ndani ya nchi, kama taifa tutakuwa tumeokoa nguvu kazi ya taifa inayoelekea kupotea kwani watoto walio wengi wanakosa fursa ya kupata elimu ingawa ni haki yao ya msingi kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

“Mimi nimefarijika kuona watoto wamewekewa utaratibu wa kupatiwa elimu hasa ukizingatia watoto wote ninao waona hapa bado wana umri mdogo na wanastahili kusoma shule.”alisema.

Alisema ataendelea kutoa msaada kwa kituo hicho kulingana na mahitaji ili nguvu kazi hiyo isije toweka na kujiingiza kwenye janga la uvutaji bangi, dawa za kulevya na ujambazi.

Kwa upande wake Baba Askofu wa kanisa la Pentekoste Jimbo la Tabora Askofu Marco Maganga Katamija ambaye ni Katibu wa Kituo alisema kituo hicho kipo chini ya Kanisa hilo na kilianzishwa mnamo mwaka 2005.

Askofu Katamija alisema chanzo cha kituo hicho kilitokana na mke wake Mama Mchungaji Naomi Katamija kuoteshwa ndoto ya kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu na yatima.

No comments:

Post a Comment