WATOTO 270 waliotokea katika mazingira magumu na familia masikini wanaolelewa na kituo cha huduma ya mtoto Bethel student center TZ -100 wamefanikiwa kupata ufadhili wa huduma za elimu,kimwili,kiroho ,kijamii na kiuchumi hali ambayo imewafanya kujikomboa katika hali ngumu ya maisha.
Hayo yalisemwa na mchungaji mwenza wa askofu Oral Sos wa kanisa la TAG Bethel Christian center mchungaji Zadock Makenzi alipokuwa akizungumza katika mahafali ya kwanza ya kuwaagavijana wa huduma ya mtoto walioamaliza muda wao ambapo jumla ya wahitimu 60 walitunukiwa vyeti vyao.
Mchungaji Makenzi alisema kuwa kituo hicho ambacho kipo chini ya shirika la compassion limekuwa likiwalea watoto walio na umri wa miaka 3 -22 na kwamba huduma zinazotolewa zimewasaidia vijana wanaoelewa hapo kupata fani ambazo zimewafanya kuweza kujiingizia vipato na hivyo kuondokana na hali ngumu ya uamsikini.
Aliongeza kuwa pia kutokana na huduma ya mtoto zipo familia ambazo tayari zilishajengewa nyumba mara baada ya nyumba za wazazi wao kupata majanga mbali mbali.
Awali meneja program wa makanisa ya washirika wenza katika shirika la Compassion Cuthbert Mono alisema kuwa huduma hiyo ambayo ipo chini ya shirika la hilo imekuwa likihudumia watoto maeneo ya elimu,uchumi,na wamekuwa wakishirikiana na makanisa katika eneo la kijamii ili kuhakikisha kuwa wanatatuliwa matatizo wanayokabiliana nayo.
Mono alisema kuwa kituo hicho kimesaidia kuwafungua sana watoto na vijana ambao wapo katika hali ya uamsikini na kwamba hadi sasa mikoa 16 ya hapa nchini inatoa huduma hizo na hadi ifikapo mwaka 2020 wanatarajia huduma ya mtoto ifike nchi nzima.
Alieleza kuwa shirika la compassion hadi sasa limefanikiwa kujenga nyumba za watoto waliopata majanga ya mafuriko kwa kipindi cha mwaka 2012 zipatazo 52 zenye thamani ya dola elfu tano katika maeneo ya Dodoma na mpwapwa lengo likiwa ni kuhakikisha watoto hao wanaishi maisha sawa na jamii nyinginezo.
Aidha katika mahafali hayo vijana 60 waliokaa kituoni kwa miaka 22 wamehitimu fani mbali mbali kama waalimu,waandishi wa habari,wahasibu,mwanasheria, boharia pamoja na hotelia
No comments:
Post a Comment