CUBA GOODING JR.
Mcheza sinema huyu aliyezaliwa Januari 2, 1968 jijini New York, leo
anatimiza miaka 47. Alitwaa Tuzo ya Academy kama Mwigizaji Bora
Mshirika (Best Supporting Actor) kwa ushiriki wake
kwenye filamu ya Jerry Maguire. Pia aliigiza kama Abraham Lincoln Haines katika
filamu ya mwaka 1992, Gladiator, na kama Meja Emanuel Stance kwenye filamu ya Red
Tails.
Alisoma
katika shule nne tofauti za sekondari na alikuwa rais wa darasa katika shule
tatu kati ya hizo. Aling’ara katika filamu za Boyz n the Hood na Radio.
Baba yake, Cuba Gooding Sr., alikuwa mwimbaji kiongozi wa The Main
Ingredient. Ana watoto watatu kwa mkewe Sara Kapfer, aliyemuoa mwaka 1994. Mwaka
2014, wanandoa hao walitengana baada ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka 20.
Aling’ara kwenye filamu ya futuhi ya Rat Race ya mwaka 2001 akiwa na Seth Green.
TIA CARRERE
Mwigizaji huyu alizaliwa mwaka 1967, tarehe kama ya leo, huko Honolulu,
Hawaii. Alipata umaarufu kwa ushiriki wake kwenye filamu ya Wayne's World. Aliigiza kama Kate Parks katika filamu ya Collision
Course ya mwaka 2012.
Wakati
akiwa na miaka 17, yaani mwaka 1985, alitolewa kwenye mchujo wa Star Search. Aliigiza kama Sydney
Fox kwenye filamu ya Relic Hunter.
Aliolewa
na Simon Wakelin mwaka 2002, na wawili hao wakapata binti
mwaka 2005 kabla ya kutalikiana mwaka 2010. Alipata umaarufu zaidi
kwenye tamthiliya ya General Hospital. Kabla yeye hajawa
maarufu, John Stamos alicheza
kama Blackie Parrish kwenye shoo hiyo hiyo.
TAYE DIGGS
Mcheza filamu huyu Mmarekani mwenye asili ya Afrika alizaliwa Januari 2,
1971 huko New Jersey. Alishiriki katika filamu za Rent na How Stella Got
Her Groove Back. Kazi zake nyingine zinazojulikana ni pamoja na Chicago, Cake,
Days of Wrath, na The Wood.
Alipata
kufanya kazi kama dansa huko Tokyo Disneyland. Alianza
kushiriki tamthiliya mwaka 1996 akicheza kama Stephon katika New York
Undercover. Alicheza kama Dr. Sam Bennett kwenye
mchezo wa runinga wa Private Practice.
Alimuoa
mwigizaji mwenzake wa Rent, Idina Menzel mwezi
Januari 2003. Ana mtoto mmoja. Filamu ya Rent ndiyo iliyompatia umaarufu mkubwa.
LOIC REMY
Mwanasoka wa Ufaransa anayechezea klabu ya Queens Park Rangers
aliyojiunga nayo mwaka 2013 akitokea Marseille. Alizaliwa Rillieux-la-Pape, nchini
Ufaransa Januari 2, 1987. Mwaka 2009 aliitwa kwenye timu ya taifa ya Ufaransa.
Alianza soka akiwa na miaka 12 katika klabu ya Lyon. Alifunga mabao 26
katika klabu ya Nice aliyoichezea tangu mwaka 2008 hadi 2010.
BARRY GOLDWATER
Mwanasiasa wa Marekani aliyezaliwa Arizona Januari 2, 1909. Alifariki
Mei 29, 1998 akiwa na miaka 89. Alikuwa mfanyabiashara mkubwa na akawa seneta
wa Arizona kwa vipindi vitano kupitia Chama cha Republican ambacho mwaka 1964
kilimteua kuwania urais. Alifahamika kwa kazi yake nzuri ya sera ya ulinzi
kwenye Senate.
Alianza
kusimamia biashara ya familia japokuwa hakuwa na uhusiano wowote na baba yake. Alianguka kwenye uchaguzi wa urais akishindwa na Rais Lyndon B Johnson ambaye, akitumia mbinu ya kuhimiza amani
kufuatia kuuawa kwa Rais John F. Kennedy, alipata asilimia kubwa zaidi katika
historia ya urais Marekani.
Mwanawe,
Barry Goldwater, Jr., alikuwa mjumbe wa Bunge la Congress wa kwanza kuwa pamoja
na baba yake.
Kutokuwa kwake maarufu kulimkosesha urais tofauti na mwenzake Lyndon B Jackson,
ambaye alifuata umaarufu wa John F Kennedy.
OSCAR MICHEAUX
Mwandishi huyu wa vitabu alizaliwa Januari 2, 1884 huko Illinois,
Marekani na alifariki Machi 25, 1951 akiwa na miaka 67. Alikuwa mwandishi wa vitabu na michezo
ya kuigiza ambaye aliandika riwaya ya The Conquest, ambayo
baadaye akaitengenezea filamu ya The Homesteader.
Filamu
nyingine, ambazo zinalenga maisha ya Waamerika Weusi, ni pamoja na Within Our
Gates (1920) na The Conjure Woman (1926).
Kabla ya
kuwa maarufu alikuwa mhudumu jijini Chicago. Baadaye,
baada ya kufanya kazi katika kampuni ya reli kwa muda, akawa homesteader jijini
South Dakota. Baadhi ya kazi zake za kwanza zilichapishwa kwenye gazeti
la The Chicago Defender.
Baba yake
alizaliwa katika utumwa huko Kentucky, na Micheaux na
nduguze 12 walikulia kwenye shamba huko Metropolis, Illinois. Alimuoa Orlean McCracken.
TOMMY MORRISON
Bondia huyu alizaliwa Januari 2, 1969 huko Arkansas na alifariki
Septemba 2, 2013 akiwa na miaka 44. Akifahamika kwa jina la utani la "The
Duke", alikuwa Bingwa wa Dunia wa WBO katika uzani wa juu tangu Juni 1993 hadi
Oktoba 1993, na anafahamika kwa ushiriki wake wa filamu ya Rocky V.
Aliingiza
kwenye mashindano ya kutunisha misuli akiwa na miaka 13 tu akitumia jina la
bandia. Alistaafu ndondi baada ya kugundulika kuwa na virusi vya Ukimwi mwaka
1996 kabla ya kujaribu kurejea mwaka 2006. Kaka yake mkubwa na baba zake wawili
wadogo wote walikuwa mabondia. Mwaka 1993 alimtwanga kwa pointi nyingi mkongwe George Foreman na
kutwaa taji la uzani wa juu duniani la WBO ambalo lilikuwa wazi.
ALICE MARY ROBERTSON
Mwanasiasa huyu aliyezaliwa Oklahoma Januari 2, 1854 alikuwa mwanamke
wa pili katika historia kuingia kwenye Bunge la Congress mwaka 1921. Alikuwa
mtetezi mkubwa wa masuala ya Wamarekani wa asili (Native American) wakati
alipoiwakilisha wilaya ya pili ya Oklahoma. Alifariki Julai 1, 1931 akiwa na
miaka 77.
Kwa miaka
sita aliwahi kufanya kazi Washington D.C katika Ofisi ya Masuala ya India, na
baada ya hapo akapewa nafasi ya peke yake kwenye Himaya ya India nchini humo.
Pamoja na
kushiriki kwenye Congress wakati wa kupitisha Marekebisho ya 19 ya Katiba
yaliyowapa haki wanawake kupiga kura, lakini yeye alipinga makundi ya wapigania
haki wanawake. Alizaliwa kwenye Misheni ya Tullahassee huko Creek Nation, sehemu ya Himaya ya Kihindi
ambayo baadaye ikaja kujulikana kama Jimbo la Oklahoma.
No comments:
Post a Comment