Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 1 January 2015

COASTAL UNION YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA JKT RUVU


NA OSCAR ASENGA, TANGA
TIMU ya Coastal Union imeanza maandalizi kabambe ya kuhakikisha inajipanga vema ili kuhakikisha timu hiyo inapata pointi tatu muhimu kwenye mechi yake ya Ligi kuu dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Jumamosi wiki hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kutokana na umahiri wa kikosi cha timu hiyo.



Akizungumza  leo mara baada ya kumalizika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wao dhidi ya Tanzania Prison tayari Kocha wao mkuu Mkenya  James Nandwa alikwisha kuyafanyia kazi na sasa kikosi kipo kamili kuwavaa maafande hao.

Amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni mzuri kwa sababu tayari,Kocha Mkuu wa timu hiyo,Mkenya James Nandwa alikwisha fanyia kazi kubwa ya kukiandaa timu hiyo na ataingia kwenye mechi hiyo akiwa na lengo moja la kuhakikisha ushindi unapatikana ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara.

Hata hivyo amesema hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ni majeruhi na kuwataka wapenzi na mashabiki kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kwenye mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

No comments:

Post a Comment