Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya (kushoto) akimkaribisha
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe katika ofisi za Mkoa huo zilizopo
mjini Kigoma wakati Waziri Chikawe na maafisa wake walipofanya ziara ya kikazi
katika mkoa huo. Waziri Chikawe alikutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
mkoa huo ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya usalama katika wilaya zote
za mkoa huo. Waziri Chikawe katika ziara yake hiyo, pia anatarajiwa kutembelea
Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo.
Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Ukumbi wa Ofisi yake. Kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe ambaye pia alishiriki katika kikao hicho kilichokuwa kinajadili masuala mbalimbali ya usalama mkoani Kigoma. Waziri Chikawe na maafisa wake waliwasili mkoani hum leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Waziri Chikawe licha ya kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo pia anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watano kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma. Watatu
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya. Waziri
Chikawe pamoja na kamati hiyo walifanya kikao kilichofayika katika Ukumbi wa
Mikutano wa ofisi za Mkoa wa Kigoma, wakijadiliana masuala mbalimbali ya Ulinzi
na Usalama ndani ya mkoa huo. Waziri Chikawe na maafisa wake waliwasili mkoani
humo leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Waziri Chikawe licha ya kukutana na Kamati hiyo, pia anatarajiwa kutembelea Kambi
za Wakimbizi zilizopo mkoani humo. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akiwasalimia waimba
kwaya wakimbizi kutoka nchini Kongo waliopo katika Kituo cha Mpito cha
Wakimbizi (NMC) kilichopo mjini Kigoma. Waimba kwaya hao walimpokea Waziri
Chikawe kwa nyimbo mbalimbali wakati alipotembelea Kituo hicho cha mpito. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole. Waziri Chikawe
yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi. Kituo hicho kilichopo mjini humo kinawahifadhi
wakimbizi zaidi ya 400 wakiwemo wanaoenda kwenye matibabu, wanaoenda nchi ya tatu,
wenye matatizo ya kiusalama, na waomba hifadhi
ya muda ya ukimbizi. Picha zote na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA
MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA
NDANI YA NCHI
.jpg)

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
No comments:
Post a Comment