
Wanajeshi kumi na wawili nchini Nigeria wamepewa adhabu ya kifo kwa uasi pamoja na jaribio la mauji.
Hii ni baada ya kumfyatuliwa bunduki afisa mkuu anayeongoza operesheni ya kupambana dhidi ya kundi haramu la kiislamu la Boko Haram kati mji wa Maiduguri,kaskazini Mashariki mwa nchi, mwezi wa Mei.
Wanajeshi hao 12 walipatikana na hatia ya kumfyatulia risasi Jemedari amadu Mohammed.
Wanajeshi hao walikasirishwa na kamanda wao ambaye walimlaumu kwa kukataa kuchukua hatua baada ya msafara wao kushambuliwa.
Jeshi la Nigeria limeshindwa kuwashinda Boko Haram na wanajeshi wamekuwa wakilalamika kuwa kila wanapokabiliana na wapiganaji wa Boko Haram hawana silaha za kutosha kukabiliana nao.
Wote walikana mashtaka hayo katika Mahakama ya kijeshi mjini Abuja.
Kiongozi wa mahakama Chukwuemeka Okonkwoalisema kuwa hata kama hukumu hizi zilikuwa chini ya udhibitisho wa mamlaka ya jeshi la Nigeria, hakukuwa na shaka juu ya uzito wa kosa hilo.Hata hivyo, hakuumia.
Mwezi uliyopita, kundi la wanajeshi kaskazini masharikimwa Nigeria walikataa kupambana na Boko Haram mpaka wapatiwe vifaa bora, mmoja wao aliiambia BBC.
BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment