Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 16 September 2014

TUSHIRIKIANE KUONDOSHA MATUMIZI YA KEMIKALI ZINAZOHARIBU TABAKA LA OZONI

Dk Binilith Mahenge, Waziri wa Nchi (Mazingira)

Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dar es Salaam.
Tarehe 16 Septemba, mwaka huu Tanzania inaungana na Jumuiya ya Kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni kama ilivyoagizwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika azimio lake la 49/114 la tarehe 19 Desemba, 1994 huku kaulimbiu yake ikiwa ni ‘Ulinzi wa Tabaka la Ozoni; Jitihada zinazoendelea (Ozone Layer Protection; Mission Goes On)’.
Tarehe hiyo ni kumbukumbu ya kutiwa saini
Mkataba wa Montreal (Montreal Protocol-1987) kuhusu kemikali zinazomonyoa Tabaka la Ozoni kwa kudhibiti utengenezaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu Tabaka hilo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) zinaeleza kuwa, Mkataba huo umepata mafanikio makubwa ya kupunguza zaidi ya asilimia 98% ambapo ni takribani tani milioni 1.8 ya uzalishaji na matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Hewa ya Ozoni.
Aidha taarifa inesema kuwa, punguzo hilo limechangia katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwasababu baadhi ya kemikali zinamong’onyoa tabaka la ozoni pia husababisha kuongezeka kwa joto duniani, mfano kiasi cha kemikali kilichoondolewa katika matumizi ni sawa na takriban tani bilioni 135 za hewa ukaa na hivyo kuchangia kwa kasi kubwa katika kukabiliana na ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya tabianchi.
Matokeo ya tafiti yanathibitisha kwamba kiwango cha kemikali zinazoharibu tabaka la Ozoni angani kinaendelea kupungua na inakadiriwa kuwa iwapo jitihada za utekelezaji wa Mkataba huo zitaendelea, Tabaka la Ozoni litarudi katika hali ya kawaida ifikapo katikati ya karne hii.
Akizungumzia kuhusu mikakati ya kitaifa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa Mkataba huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mhe. Mhandisi Dkt. Mahenge alisema kuwa 1996 Serikali iliandaa na kutekeleza Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni, mikakati hiyo ni pamoja kujenga uwezo wa Taasisi zinazosimamia utekelezaji wa Mkataba, kuweka takwimu za kemikali hizo, kutoa elimu kwa wadau na kwa umma kuhusu umuhimu wa Tabaka la Ozoni na hatari zinazolikabili, kusambaza habari kuhusu kemikali na teknolojia mbadala, kubadilisha teknolojia katika viwanda vinavyotumia kemikali haribifu, kutoa mafunzo yanayolenga kuimarisha ujuzi katika sekta ya kuhudumia viyoyozi na majokofu.
Mikakati mingine ya kitaifa ni kuimarisha mbinu za upunguzaji wa matumizi ya kemikali husika kwa kuanzisha mtandao wa kunasa, kusafisha na kurejeleza vipoza joto, kuhamasisha na kuhimiza matumizi ya kemikali na teknolojia mbadala na rafiki kwa tabaka la Ozoni pamoja na kuweka taratibu za kudhibiti uingizaji na matumizi ya kemikali zinazodhibitiwa na Mkataba wa Montreal.
“Hatua hizi zimewezesha Tanzania kuondosha kemikali hizi kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa na Mkataba”, alisema Dkt. Mwandisi Mahenge.
Dkt. Mahenge alibainisha kuwa Chini ya Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali haribifu, serikali iliandaa Mpango wa Usimamizi wa Vipodozi yaani (Refrigerant Management Plan) na katika utekelezaji wake, mambo kadhaa yamefanyika ikiwemo kuandaa Kanuni za Usimamizi wa kemikali zinazomong’onyoa tabaka la hewa ya Ozoni ambazo zilianza kutumika tarehe 7 Desemba mwaka 2007.
Pia kusambaza kwa Vitambuzi vya kemikali hizo vipatavyo 18 kwa ajili ya vituo vilivyo mipakani mwa Tanzania, pia kusambaza mitambo na zana za kuhudumia majokofu na viyoyozi kama vile mashine za kunasa na kurejeleza gesi chakavu kwa vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya fani ya kuhudumia majokofu na viyoyozi hapa nchini. 

No comments:

Post a Comment