(Picha zote kwa hisani ya JamiiForums)
Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo unaendelea pale Mlimani City jijini Dar es Salaam ambao utamchagua Mwenyekiti pamoja na makamu wake wa Bara na Zanzibar.
Pia jana vikao vikuu vya chama - Kamati Kuu na Baraza Kuu vimefanyika.
Mkutano wa leo umeanza rasmi tangu saa 4 asubuhi ambapo waalikwa mbalimbali wamehudhuria wakiwemo Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula, Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, mabalozi mbalimbali na viongozi wa vyama rafiki wa Chadema kutoka nchi mbalimbali.
Tutaendelea kuwaletea yanayojiri...

No comments:
Post a Comment