SHIRIKA LA HUC LATANGAZA UFADHILI WA MASOMO YA UFUNDI
VETA, VIJANA CHANGAMKIENI
Na Nathan
Mpangala wa HUC.
Shirika
lisilo la kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC), linatangaza
nafasi za ufadhili wa masomo ya ufundi VETA kwa vijana wa Kitanzania. Kozi hizo
ni ufundi wa magari, umeme wa magari, udereva magari/pikipiki, ufundi
cherehani, hair dressing (urembo), mapambo ya ukumbi na nyinginezo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo, inasema, HUC, itafadhili
wanafunzi 15 wa kozi mbalimbali za awali VETA kwa mwaka 2014-2015.
Walengwa
ni vijana wa kike na kiume waliomaliza shule za msingi ambao wamethibitika kuwa wazazi/walezi wao
wameshindwa kuwalipia ada. Imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa
hiyo imeongeza kuwa, mwanafunzi atatakiwa kujaza kwa usahihi fomu ya maombi (imeambatanishwa hapa),
akiambatanisha na barua akieleza sababu za kuomba ufadhili huu na barua ya
utambulisho toka ofisi ya serikali za mitaa na mwisho wa kupokea barua za maombi
ni Jumatano, Oktoba 01, 2014, saa 11 jioni.
Barua za maombi zitumwe kupitia:
Maombi ya ufadhili wa masomo,
Help for Underserved Communities Inc.
P. O. Box 7022,
Dar es Salaam,
Tanzania.
Au
Help for Underserved Communities Inc.
P.O.Box 6822,
Ellicott City, MD 21042
Au
Kupitia baruapepe:
Taarifa
hiyo imesema, majina ya watakaopata ufadhili yatatangazwa Oktoba 10, 2014 na
kwamba ada italipwa moja kwa moja chuoni.
HUC ni shirika
lisilo la kiserikali toka nchini Marekani lenye lengo la kuziwezesha jamii
zipatazo huduma hafifu kupata maji safi na salama, vifaa vya elimu na ufadhili
wa masomo ya ufundi. Mwaka jana, shirika
hili lilifadhili vijana 11 VETA.
XXXXXXXX
Regards,
Nathan Mpangala
Editorial Cartoonist | Comic Artist | Illustrator | Animator | Blogger
Editorial Cartoonist: ITV Tanzania
Founder: Wafanye Watabasamu Initiative
P. O Box 7022,
Dar es Salaam,
TANZANIA.
Phone: +255 713 262 902
No comments:
Post a Comment