Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 8 September 2014

SERIKALI YALIPA DENI LA WALIMU SHS. 44 BILONI


Serikali imetumia Shilingi 44 bilioni kwa ajili ya kupunguza kulipa madeni mbalimbali inayodaiwa na walimu wakiwamo wa shule za msingi na sekondari huku ikisema hatua hiyo ni sehemu ya kuwapunguzia makali ya maisha.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (Tamisemi) anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa, wakati akizungumza na wakuu wa Shule za sekondari wa mkoa wa Lindi katika mji mdogo wa Masoko,wilaya ya Kilwa.

Majaliwa alisema madeni hayo yalianza kulipwa katikati ya mwaka uliopita na kuendelea hadi hivi sasa.

Akasema ili kufikia malengo ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika utendaji na uwajibikaji, Serikali imeanza kupunguza madeni ya walimu zikiwamo fedha za uhamisho, likizo, masomo na matibabu.

Majaliwa alisema kwamba hadi sasa serikali imetumia Sh. bilioni kati ya Sh. bilioni 61.0 ambazo inadaiwa na walimu sambamba na uhakiki wa madeni mengine ya walimu ambayo hayajalipwa.

“Kwa hivi sasa kazi nyingine inayoendelea ni pamoja na uhakiki wa madeni na kuwatambua wengine ili waweze kulipwa,” alisema.
Majaliwa alifafanua kuwa serikali imejipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifuko mizuri itakayowezesha watumishi kuitumia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Alisema uhakiki huo ambao ulianza mwaka jana, umeweza kubaini kuwa kiwango cha deni la Sh. bilioni 61.0 siyo sahihi  kutokana na baadhi ya madeni hayo kuonyesha kujirudia.

Aliwataka walimu wakuu, maofisa elimu na wakurugenzi wa halmashauri kusimamia vema matumizi ya fedha za ruzuku zinazotolewa na Serikali ili kuhakikisha zinafika mashuleni na kutumika kama inavyokusudiwa.

Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, mkoani Lindi, alisema Serikali haitasita kuwafukuza kazi watumishi watakaobainika kufuja fedha hizo ili kukomesha tabia hiyo ambayo inachangia kuzorotesha na kupunguza kasi katika sekta ya elimu.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment