NA MASHAKA MGETA
Mbunge wa Nzega kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Hamisi Kigwangalla, ametangaza nia ya kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao, huku akiahidi kukabiliana na ukosefu wa uwajibikaji unaochangia ongezeko la ufisadi na kwa vitendo vinavyohujumu uchumi wa nchi.
Dk. Kigwangalla ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, amesema ili kurejesha misingi ya uwajibikaji nchini, atabadilisha mfumo wa vipaumbele na uendeshaji wa serikali ikiwa atateuliwa na CCM na hatimaye kushinda katika uchaguzi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Dk. Kigwangalla, alisema nia ya kuwania urais imetokana na utashi binafsi pasipo msukumo wa asasi za kiaraia ama kikundi cha watu wanaojenga mitandao ya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani.
Kwa mujibu wa Dk. Kigwangalla, hatua ya kutangaza nia nje ya jimbo lake (Nzega), ilitokana na ukweli kwamba nafasi anayoiomba ni ya kitaifa, hivyo kuwa na uhuru wa kufanya hivyo katika eneo lolote la nchi.
Hata hivyo, alisema wapo watu wa kada na itikadi tofauti wanaomuunga mkono na ambao hivi sasa, hawatajitokeza ili kuepuka kuonekana ameanza kampeni, jambo lililo kinyume cha sheria za nchi.
Alisema hivi sasa taifa linakabiliwa na matendo yanayoashiria ukosefu wa haki na usawa, hali inayosababisha kuwapo pengo kati ya matajiri na masikini.
Kwa mujibu wa Dk. Kingwangalla, maeneo mengine yanahusu unyanyasaji dhidi ya vijana na wanawake wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo na ukosefu wa huduma bora za jamii katika maeneo mengi ya nchi.
Alisema kutokana na hali hiyo, taifa linahitaji Rais aliyejipima na pasipo kushawishiwa, akatumia utashi wake kuamua kuwania nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa nchi.
“Mnawasikia wapo wenye ndoto walioianza safari ya matumaini, wengine wanasubiri kuoteshwa na wengine wanadai kutumwa ili wagombee Urais…mimi nimejipima na kwa utashi wangu nimeona ninafaa kuwa Rais wa nchi hii,” alisema. Kwenye mkutano huo, Dk Kigwangalla alifuatana na wazazi wake, Nasser Kigwangalla na mama yake, Bagaile Bakari, mkewe, Dk Bayun Awadhi na watoto wake, Sheila, Hawa na HK Junior, baadhi ya ndugu, marafiki na makada wa CCM.
AKOSOA UTENDAJI, UWAJIBIKAJI
Pamoja na kusifia utendaji kazi wa serikali ya CCM katika awamu zote, Dk. Kigwangalla, alisema mfumo wa vipaumbele na mtindo wa uendeshaji wa serikali vinapaswa kubadilishwa ili kuifanya Tanzania, pamoja na mambo mengine, iondokane na umasikini ikiwamo kupitia rasilimali zake.
Alisema baadhi ya watendaji serikalini wamekuwa na kasumba ya kufanya kwa mazoezi, huku wakishiriki vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na kuathiri uchumi wa nchi na watu wake.
AKUMBUSHIA SAKATA RICHMOND, EPA
Dk. Kigwangalla, alidai kuwa ukosefu wa uwajibikaji kwa wanaofanya maovu serikalini, ulichangia kuwapo kwa kashfa kama zile za Richmond na EPA na kusema wahusika wake hawakuchukuliwa hatua stahiki.
Hata hivyo Dk. Kigwangalla, alisema kama wahusika wa Richmond na EPA wangefungwa, kile alichokiita kuwa ni wizi uliofanyika kwenye kampuni za IPTL na kashfa ya akaunti ya Escrow, visingetokea.
“Kama waliotuingiza katika kashfa za Richmond na EPA wangefungwa, huu wizi wa Escrow na IPTL usingetokea, wangeogopa kufungwa,” alisema.
Hivi karibuni, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR), David Kafulila, aliliambia Bunge mjini Dodoma kuwa ana ushahidi wa wizi wa Dola milioni 270 katika akaunti ya Tegeta Escrow na Dola milioni 122 zilizokwishatolewa na kupewa kampuni ya PAP. Sakata hilo lilihusisha kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL) ambayo imeshamfunguliwa kesi mbunge huyo, huku ikimtaka awalipe fidia ya Sh. bilioni 310.
AELEZA ALIVYOUISHI UMASIKINI
Dk. Kigwangall, alijinasibu kuwa mmoja wa watu walioushi umasikini ndani ya familia masikini na ambayo ilishindwa kumudu gharama za masoko ikiwamo kumnunulia mahitaji muhimu.
Alisema, pamoja na ukweli huo, alijiwajibisha katika elimu, akapitia hatua tofauti hadi kuhitimu taaluma ya udaktari na baadaye kuwa Mbunge, hali inayompa nguvu ya kuwa kiongozi anayefaa kushughulikia umasikini uliopo nchini.
Kwa hali hiyo, alisema ikiwa atateuliwa na CCM kisha kushinda nafasi hiyo, miongoni mwa nyenzo atakazozitumia ni kubadilisha sheria kandamizi na zile zinazotoa mianya ya kufanyika kwa unyanyasaji, ubadhirifu wa rasilimali, ufisadi na mambo mengine yanayokwamisha upatikanaji wa huduma muhimu za jamii.
Dk. Kigwangalla anakuwa mwanachama wa pili wa CCM kutangaza hadharani nia ya kuwania urais, huku wengine wakitoa kauli zinazohusishwa kwa namna tofauti kutaka kugombea nafasi hiyo.
Wa kwanza ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, aliyetangaza nia yake wakati akizungumza kwenye mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) Idhaa ya Kiswahili Julai 2, mwaka huu akiwa safarini nchini humo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amedaiwa kutangaza nia alipokutana na baadhi ya viongozi wa CCM mkoani Mwanza takribani wiki tatu zilizopita , lakini hadi sasa si yeye ama ofisi yake iliyothibitisha ama kukanusha taarifa hiyo.
Mtangulizi wake, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, aliwahi kutangaza ndoto yake kuhusu safari ya matumaini kwa Watanzania, ambayo hata hivyo ilihusishwa na ‘mbio’ za urais wa 2015. Majina mengine yanayotajwa ni pamoja na Bernard Membe (Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa).
Wengine ni Stephen Wassira (Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu), Samuel Sitta (Afrika Mashariki) Asha-Rose Migiro (Katiba na Sheria) na Anna Tibaijuka (Ardhi, Nyumba na Makazi), wabunge William Ngeleja (Sengerema), Emmanuel Nchimbi (Songea Mjini) na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
Makada sita Lowassa, Sumaye, Wassira, Makamba, Ngeleja na Membe walihojiwa na kupewa karipio na kufungiwa kwa miezi sita kujihusisha na shughuli za chama kutokana na kile ambacho Kamati Kuu ilikiita kuanza kwao kampeni za urais kabla ya kuda rasmi.
Makada hao waliohojiwa Februari mwaka huu, walipewa angalizo kuwa wakibainika kukaidi watachukuliwa hatua zaidi ambazo hata hivyo, Kamati Kuu haikuitaja.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment