Scotland imefanya uamuzi wa mwisho kuwa itaendelea kubaki sehemu ya Uingereza , raia kwa pamoja wamekataa uhuru wa Scotland.
Maeneo 31 kati ya 32 wamepika kura ya HAPANA siku ya Alhamisi na kuongoza kwa kura 1,914,187 dhidi ya 1,539,920.
Ushindi huo ni asilimia 55 dhidi ya 45
waliokuwa wakiunga mkono hatua ya kujitenga.
Waziri Kiongozi wa Scotland Alex Salmond amesema ameridhia kuanguka katika mchakato wa kura ya maoni.
Jana Alhamisi, wapiga kura walijitokeza katika maeneo mbali mbali nchini Scotland, ili kuamua ikiwa wataendela kuwa sehemu ya Uingereza au wawe taifa huru kwa mara ya kwanza kabisa tangu zaidi ya miaka 300 iliyopita.
Jana kulikuwa na shughuli nyingi katika historia ya kupiga kura eneo la Scotland ambapo asilimai 97 ya watu walikuwa wamejiandikisha kupiga kura.
Awali kulikuwa na kampeni kali katika saa 24 kabla ya upigaji kura huku ikidhihirika matokeo yanaweza kwenda upande wowote.
Kiongozi wa chama cha Scotish National Party, Alex Salmond, alitaja kampeni ya kuitisha Uhuru wa Scotland kutoka kwa Uingereza kama tukio muhimu zaidi la kidemokrasia kuwahi kutendeka nchini humo.
Kadhalika alisema tayari limebadilisha mfumo wa maisha eneo la Scotland.
Idadi kubwa ya wapiga kura wamesajiliwa na kwa mara ya kwanza vijana wenye umri wa miaka 16 na 17 waliruhusiwa kupiga kura.
CREDIT: BBC/SWAHILI

No comments:
Post a Comment