
Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA), limewaambia viongozi wanaounda kamati ya utendaji na viongozi wengine wa juu wa shirikisho hilo kurejesha saa zipatazo 65 za gharama walizopokea kama zawadi kipindi cha kuelekea Kombe la Dunia huko Brazil mwaka huu.
FIFA imesema kitendo cha kurejesha saa
hizo ni kutunza nidhamu.
Saa hizo zinakadiriwa kuwa na gharama ya Dolla 25,000 (takriban TShs. 40 milioni) kila moja na zinatakiwa zirudishwe Oktoba 24, mwaka huu.
Saa hizo za kumbukumbu ya Parmigiani ziligawiwa na Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) wakati wa mkutano wa maandalizi wa FIFA uliofanyika mjini Sao Paulo.
FIFA imesema kuwa kanuni za maadili zinazuia viongozi kupokea zawadi ambazo zinathamani zaidi au zenye kuonesha ishara fulani.
Inasemekana kwamba saa hizo zitatolewa kwa taasisi zinazojitegemea na si sile zinazojali maslahi huko Brazil.
CREDIT: BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment