Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 17 September 2014

RAIS KIKWETE YUKO MAREKANI KWA ZIARA YA WIKI MBILI

Rais Jakaya Kikwete

Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete ameondoka Jumatatu usiku kwenda Marekani kuanza ziara ya wiki mbili nchini humo.
Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu,
ilisema Rais atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York pamoja na kuhudhuria mikutano muhimu Washington, D.C.
Akiwa Mjini New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya 10 iliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi Oktoba Mosi. Rais Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia baraza hilo.
Septemba 25. Pia atakuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu mazingira (CAHOSC) ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki Moon.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment