Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 17 September 2014

BARAZA LATAKA LUGHA MOJA KUFUNDISHIA WANAFUNZI NCHINI


Mwenyekiti wa TACELAM, Cheleztino Mofuga (kulia) na Katibu wake, Dk Newton Kyando walipokuwa akitoa taarifa ya kongamano hilo

Serikali imeshauriwa kutumia lugha moja ya kufundishia kuanzia elimu ya awali hadi vyuo vikuu ili kuwavutia wanafunzi kusoma kwa bidii hasa masomo
ya sanyansi na kupata wataalam wa sekta mbalimbali nchini.

Ushauri huo umetolewa na Ofisa wa Baraza la Elimu la Uongozi, Utawala na Usimamizi wa Elimu Nchini (TACELAM), Chelestino Mofuga wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.

Mofuga alikuwa akizungumzia kuhusu kufanyika kwa  kongamano la kujadili sayansi, teknolojia, afya,  mazingira, usalama,  amani na kuimarisha mfumo wa kujifunza masomo ya sayansi litakalofanyika Chuo Kikuu Mkwawa mkoani Iringa kuanzia Oktoba 4 hadi 6, mwaka huu.

“Ingetakiwa kuweka lugha moja ya kufundishia, mwanafunzi anaanza kusoma Kiswahili baadaye Kingereza hii inakuwa ngumu mwanafunzi kupenda shule, ” alisema Mofuga

 Awali Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Newton Kyando,  alisema kuwa kongamano hilo linatarajiwa kuimarisha mfumo wa maendeleo wa kujifunzia wanafunzi kuanzia shule za awali  hadi vyuo vikuu.

Kyando, alisema kuwa wameandaa kongamano hilo baada ya kubaini kuwa walimu wanaojiriwa  kufundisha hawana mwamko mzuri wa kufundishaji masomo ya sayansi na kusababisha wanafunzi wengi kuyakimbia kutokana na kufanya vibaya katika mitihani yao.

“Kama mwanafunzi hana mwamko wa kusoma akikutana na mwalimu ambaye hana ujuzi wa kufundisha basi hapo hakuna hata mmoja atakayemuelewa na matokeo yake ni wanafunzi kuchukia kusoma Sayansi, ” alisema Kyando

Aliitaka Serikali na wadau wa elimu kuandaa mitaala ya elimu ambayo itawafundisha wanafunzi kujitegemea na siyo kusubiri iwaajiri.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment