Rais Dk. Jakaya Kikwete
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wenye vyeo vya Brigedia Jenerali kuwa Meja Jenerali.
Taarifa hiyo ilisema Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange aliwavisha vyeo maofisa hao kwa niaba ya Rais Kikwete katika sherehe zilizofanyika jana katika Makao Makuu ya JWTZ.
Waliopandishwa vyeo ni pamoja na Gaudence Milanzi, James Mwakibolwa, Ndetaulwa Zakayo, Venance Mabeyo, Simon Mumwikuwa, Issa Nassor na Rogastian Laswai.
Taarifa hiyo ilisema Meja Jenerali Milanzi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC). Nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Luteni Jenerali Charles Makalala ambaye amestaafu.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment