Kwenye picha ni baadhi ya madawati yaliyotolewa na Meya wa Ilala Mstahiki Jerry Silaa katika shule ya Kivule
iliyopo Manispaa ya Ilaa jijini Dar es Salaam
iliyopo Manispaa ya Ilaa jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wanaendelea kusikiliza tukio linavyoendelea
Kikundi cha ngoma cha makirikiri kilichoundwa na wanafunzi kwaajiri ya kusherehesha katika sherehe hiyo ua kukabidhi madawati katika shule ya Kivule
Burudani ikiwa imepamba moto
kundi la burudani ka kikulwa likiwa linatoa burudani wakati wa kukabidhi madawati hayo
Mh:Jerry Silaa akiwa ameongozana wa viongozi mbalimbali walio kuwepo katika shughuli hiyo kwenda kukagua madarasa mawili mapya yaliyo jengwa hivi karibuni
Akizungumza na viongozi hao mara baada ya kuangalia madarasa hayo ambayo nayo ameshirika katika kuchangia wakati wa ujenzi
Haya ndiyo madarasa ya vyumba viwili mapya yaliyo jengwa hivi karibuni katika shule ya Kivule
Akikabidhi madawati hayo, Silaa amewaasa kuwa hata yeye alikuwa anasoma na anakaa chini lakini kwa kizazi cha sasa yatupasa tubadilike hiyo hatapenda kuona watoto wakiendelea kukaa chini na kusoma katika mazingira magumu kama aliyo weza kusoma yeye kwahiyo kwa moyo wake anarudisha fadhira kwa watanzania kwa kushirikiana na wadau mbal;imbali kwa misaada tofautitofauti katika kipindi chake cha uongozi kwa nafasi ya meya.
Aidha muheshimiwa aliweza kuwafafanulia baadhi ya watu walio weza kufika katika hafra ya kukabidhi madawati kwa shule ya kivule kwamba kodi za pango zinavyo kusanywa huwa haziliwi na mtu zaidi ya kutatua matatizo katika sehemu mbalimbali ya halmashauri kwahiyo aliwaomba watu wote wasiwe na imani ya kuliwa kwa fedha hizo bali watambue zinakazi nyingi na tofauti tofauti katika halmashauri husika.
Naye mwalimu mkuu wa shule ya kivule wakati akisoma risala waliyo iandaa kwaajiri ya shughuli hiyo alisema shule ya kivule inawanafunzi wengi ambao ni takribani ya wanafunzi 2020 ambapo inakabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa madawati ,matundu ya vyoo,nyumba za walimu ambapo kwa sasa kuna nyumba moja tu,waalimu wa masomo mbalimbali pamoja na vifaa vya kufundishia hususani somo la Tehama, hivyo kupelekea waalimu kutumia nguvu katika ufundishaji.
Bw.kubilu Lupembe Dede ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya kivule ametoa shukrani za dhati kwa mstahiki meya wa Ilala Jerry Silaa ambapo ameonesha nia ya dhati katika kufanikisha elimu inasonga mbele kwa kujitoa sehemu mbalimbali na kuwa karibu na jamii.
Pia diwani wa kata ya kivule Bw.Nyansika.G.Motena ametoa shukrani kwa niaba ya wananchi wote kwa kile anacho kifanya mheshimiwa meya wa ilala Jerry Silaa ameweza kukifany ana kusema inapaswa kuwa kiongozi wa mfano kwa wengine.
CREDIT: FULLSHANGWE BLOG
No comments:
Post a Comment