Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amewata viongozi wa serikali na Chama kuacha tabia kujilimbikizia vyeo na kuvitumia kama kinga.
Badala yake amewataka wawaachie wanachama wenye sifa kushika
nyadhifa hizo.Kinana alitoa wito huo hapa jana aliposomewa taarifa ya Chama na Serikali baada kuwasili mkoani Pwani kwa ziara yake ya siku 30 katika mikoa ya Pwani, Tanga na Tabora.
Alisema ni vyema viongozi wakaacha kung'anga'ania vyeo na matokeo yake kushindwa kutimiza majukumu ya kuwatumikia wananchi na kutumia vyeo kama utukufu badala ya utumishi.
“Ni vyema viongozi wenye vyeo vingi kuviachia kwa hiari yao, badala ya kuving'ang'ania na matokeo yake wanashindwa kutimiza majukumu waliyopewa ya kutumikia wananchi. Msitumie madaraka kama miavuli ya kuficha maovu yenu,” alisema.
Kauli hiyo ya Kinana ilifuatia taarifa iliyowasilishwa kwake na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao, kulalamikia viongozi wa kamati mbambali za chama kutohudhuria vikao vya Chama kutokana na kubanwa na majukumu mengine.

CHANZO: NIPASHE
.jpg)
No comments:
Post a Comment