
Na Sosthenes Nyoni na Vicky Kimaro, Mwananchi
Jumatatu,Septemba15 2014
Dar es Salaam. Mshambuliaji Genilson Santana
‘Jaja’ jana alikuwa na kazi moja ya kunyamazisha wanaombeza baada ya
kufunga mabao mawili na kuiongoza Yanga kuichapa Azam 3-0 katika mchezo
wa Ngao ya Jamii kwenye Uwanja Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji huyo Mbrazili alifunga mabao hayo
mawili ndani ya
dakika tisa katika kipindi cha pili na Simon Msuva akafunga bao lililohitimisha ushindi huo mnono dhidi ya moja ya timu bora nchini.
dakika tisa katika kipindi cha pili na Simon Msuva akafunga bao lililohitimisha ushindi huo mnono dhidi ya moja ya timu bora nchini.
Jaja, ambaye aliwasili msimu huu baada ya kocha
Mbrazili Marcio Maximo kuajiriwa Yanga alifunga bao la kwanza katika
dakika 56 alipounganisha krosi ya chini ya Msuva, aliyeingia kipindi cha
pili.
Mshambuliaji huyo wa kati aliongeza bao la pili
katika dakika ya 65. Alikuwa amepewa pasi upande wa kulia wa eneo la
penati. Aliufuata, akamwangilia kipa Mwadini Ali na baadaye kupiga kiki
kwa kuubetulia mpira juu ya kipa huyo ambaye alikuwa ametoka kwenye
mstari wake akiwa amebana upande wa kushoto.
Mashabiki na wachambuzi wengi wa soka wamekuwa
wakimbeza Jaja kuwa ni mchezaji mzito, lakini mabao ya jana yatawafanya
wafikirie upya uwezo wake.
Msuva alihitimisha karamu hiyo ya mabao katika
dakika ya 87. Alikuwa ametanguliziwa mpira mrefu na Hussein Javu, lakini
Mwadini alitoka vibaya golini na kurusha daruga kwa lengo la kuubutulia
mbele mpira na alipoukosa, Msuva aliufuata na ‘kuuburuzia’ mpira golini
wakati kipa huyo akigaagaa chini.
“Wachezaji walicheza vizurina wamepata matokeo
mazuri. sasa naanza maandalizi kwa ajili ya mechi ya Mtibwa Sugar
inayofundishwa na kijana wangu,” alisema Maximo baada ya mchezo.
Azam ilichezesha mshambuliaji mmoja, Didier
Kavumbangu wakati Kipre Tchetche na Leonel waliongeza nguvu katika safu
ya kiungo iliyokuwa na wachezaji watano, lakini ikamudu kutengeneza
nafasi ambazo hazikutumiwa vizuri.
“Ni vizuri kwamba tumepata matokeo haya mapema kwa
sababu yatatusaidia kujirekebisha kabla ya kuanza ligi,” alisema kocha
Mcamerooni wa Azam, Joseph Omog.
Kavumbagu, Tchetche na Leonel kupata nafasi nyingi za kupiga mashuti, lakini yaliishia mikononi mwa Dida.
Yanga ilipeleka mashambulizi mengi kupitia upande
wa kulia ambako Mrisho Ngasa na Haruna Niyonzima walikuwa wakipita
kirahisi na kutuma krosi ambazo hata hivyo hazikuunganishwa wavuni.
Mwamuzi Mbelwa alitoa kadi za njano kwa nahodha wa Azam,
Abubakari Salum na mwenzake wa Yanga, Nadir Haroub ‘Canavarro’ kwa
mchezo mbaya.
Kwa mara ya kwanza baada ya filimbi ya mapumziko winga wa Yanga, Ngasa alibadilishana jezi na Abubakari ‘Sure Boy’.
Azam FC: Mwadini, Shomari Kapombe, Erasto
Nyoni/Gadiel Michael, David Mwantika, Aggrey Moris, Bolou Michael, Himid
Mao/Khamis Mcha, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Kavumbagu, Tchetche/Ismail
Diara na Leonel Saint Preux/Kelvin Friday.
Yanga: Dida, Said Juma/Hassan Dilunga, Oscar
Joshua, Canavaro, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Said Juma,
Niyonzima/Hamis Kiiza, Jaja/Javu, Ngassa/Omega Seme na Nizar
Khalfan/Msuva.
CREDIT: MWANANCHI: KIMBUNGA JAJA CHAIKUMBA AZAM
CREDIT: MWANANCHI: KIMBUNGA JAJA CHAIKUMBA AZAM
No comments:
Post a Comment