Kiungo
wa timu ya Coastal Union, Godfrey Wambura amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa
mwezi Februari 2015 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi
kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Wambura amechaguliwa kuwa mchezaji bora baada ya
jopo la makocha linalofanya majumuisho ya wachezaji bora wa kila mchezo, ambapo
kiungo huyo ameweza kuwapiku wachezaji Saimon Msuva wa Young Africans, Abasirim
Chidiebere wa Stand United na Gideon
Benson wa Ndanda FC.
Kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi Februari,
Wambura atazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya
simu za mkononi ya Vodacom.
Jopo maalumu la makocha waliopo katika viwanja
vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya
kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo
vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.
Wakati huo huo timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga
Stars) inatarajiwa kuagwa mbele ya waandishi wa habari kesho alhamisi saa 5
kamili katika ukumbi wa TFF Karume.
No comments:
Post a Comment