
Wasimamizi wa uchaguzi nchini Nigeria wakihesabu kura
Upigaji kura uliendelea katika
siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za
kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura.
Mama akipiga kura nchini Nigeria
Kauli hiyo imetolewa na
mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, INEC, Attahiru Jega. "Tumaini letu
na ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi kwa bidii ni kuweza kutangaza
matokeo ya uchaguzi ndani ya saa arobaini na nane na tunatumaini muda
mchache zaidi kuliko ule wa mwaka 2011. Imeanza kutoka saa 48 baada ya
uchaguzi kumalizika jana. Kwa hiyo tumeanza kuhesabu saa arobaini na
nane kwa kweli kutoka jana jioni wakati idadi ya kutosha ya majimbo
yalipofanya uchaguzi."Bwana Jega amesema alitumaini jumuia ya kimataifa inaweza kupongeza namna Nigeria ilivyoendesha uchaguzi."Tunaamini tumefanya vizuri kabisa. Hatuwezi kupuuza changamoto tulizokumbana nazo. Ni hakika haukuwa kamilifu lakini tunaamini kwa ujumla tumefanya vizuri sana, japokuwa bado tunayo nafasi ya kuzidi kuuboresha. Na kwa namna yoyote ndiyo maana tuliwaalika waangalizi vikiwemo vyombo vya habari na waangalizi wengine wa uchaguzi, ili kuweza kutangaza habari na tunaweza kujifunza kutokana na ripoti hizi na tunaweza kuendelea kuboresha mchakato wa uchaguzi.", amesema Jega.

Wasimamizi wa uchaguzi wakiwahakikika wapiga kura kabla ya kupiga kura zao.
Wachambuzi wa mambo wanasema
ushindani ni mkubwa sana kiasi cha kushindwa kutamka mshindi ni nani.
Ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa Afrika umesema uchaguzi ulikuwa wa
amani lakini wamewataka wananchi wa Nigeria kukubali matokeo.CREDIT: BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment