Mchezo wa
kirafiki wa Kimataifa uliofanyika jana jumapili jijini Mwanza kwenye Uwanja wa
CCM Kirumba kati ya wenyeji timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya
timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) umengiza jumla ya tsh 72.839,000 kutokana
na idadi ya washabiki 15,762 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.
Mgawanyo wa
mapato kwa mchezo hu ni VAT 18% sh. 11,111,103, gharama za tiketi sh.
3,203,700, gharama za mchezo (15%)sh. 8,778,639, Uwanja (15%) 8,778,639, CAF
(10%) sh. 5,852,426 na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF (35%) sh.
35,114,560.
Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini inatoa shukrani kwa chama cha soka mkoa wa Mwanza (MZFA) kwa ushirikiano wao katika kufanikisha
maandalizi ya mchezo huo, waandishi na vyombo vya habari mbalimbali kwa sapoti
waliyoitoa kwa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
Aidha TFF
iinawashukru wapenzi, wadau na washabiki wa soka nchini, na hususani wa kanda
ya ziwa waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo, kwani waliishangilia
Taifa Stars tangu mwanzo wa mchezo mpaka mwisho kwa ustaarabu wa hali juu.
Katika mchezo huo
Taifa Star ilitoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya The Flames, bao la wageni lilifungwa
na Mecium Mhone kabla ya na Mbwana Samatta kuisawazishia Tanzania.
No comments:
Post a Comment