Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana.
Na Augusta Njoji, Hai
Wananchi
wa vijiji vinane vinavyopakana na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
Kilimanjaro (KIA), wametakiwa kuendelea na shughuli zao mpaka hapo
serikali itakapotafuta ufumbuzi wa mgogoro kati yao na uwanja huo.
Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Abdulrahman Kinana (pichani), kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji
cha Mtakuja wilayani humu juzi.
Kinana alisema mgogoro wa muda mrefu kati ya wananchi na kampuni
ya Kilimanjaro Airports Development Company (Kadco), unahitaji ufumbuzi
wa haraka.
Alisema atahakikisha analifikisha suala hilo katika kikao cha juu
ambacho Mwenyekiti wake ni Rais Jakaya Kikwete, ili utolewe uamuzi ya
haraka huku akisisitiza kuwa eneo wanalomiliki KIA kwa sasa bado lina
nafasi kubwa.
“Naomba mtulie na muendelee na shughuli zenu kama kawaida huku
Chama Cha Mapinduzi kikiendelea kulipeleka suala hili katika vikao vya
uamuzi wa juu," alisema Kinana.
“Niliwahi kusema sera ya ubinafsishaji si mbaya, lakini kuwauzia
watu maeneo wasiyoyatumuia si sawa, Kadco wana uzoefu wanaweza kuleta
ndege, biashara na hata ajira, lakini ninachosema watuonyeshe vizuri
hekta 460 zimetumikaje kabla hawajachukua nyingine za ziada,” alisema
Kinana.
Awali, mwakilishi wa kijiji hicho, Steven Laizer, alisoma risala
mbele ya Kinana ambayo ilijaa malalamiko dhidi ya serikali hasa Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutaka kupora eneo lao takatifu
ambalo kwa mujibu wao, ndipo jamii ya Maasai ilipoanzia.
Alisema Kadco inadai wananchi hao wamevamia ardhi yake yenye ukubwa
wa hekta 11,085, wakati siyo kweli kiuhalisia kampuni hiyo
inajaribu kuvipora vijiji hekta 11,448.
SOURCE:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment