Wakuu nchini Sierra Leone wanajiandaa kuanzisha hatua za siku tatu za kuwazuia watu manyumbani, ili kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa wa ebola na kuuangamiza kabisa.
Zaidi ya watu milioni sita wameombwa kusalia manyumbani katika kipindi cha siku tatu zijazo huku wahudumu wa kujitolea wakizuru nyumba hadi nyumba, kuwatafuta watu walio na dalili za ugonjwa huo huku wakiwafunza raia mbinu za kujizuia kupata ugonjwa huo.
Kuna visa vichache mno ambavyo vimeripotiwa kaskazini na magharibi mwa Sierra Leone juma lililopita.
Mataifa matatu ya Afrika magharibi, Sierra Leone, Liberia na Guinea yaliyoathirika pakubwa na ugonjwa huo kwa pamoja yameweka mikakati ya kuangamiza kabisa maradhi hayo hatari.
Yanasema hakutakuwepo na visa vipya vya ugonjwa huo ifikiapo katikati ya mwezi Aprili.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment