Leodegar Tenga (kushoto) na Jamal Malinzi
Jana Rais wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na
Kati (CECAFA), Leodegar Tenga na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF) akiwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi wamezungumzia uchaguzi wa CAF na FIFA.
Rais Tenga ameishukuru familia ya TFF kwa kumuunga mkono katika
kugombea tena nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF katika uchaguzi
utakaofanyika Aprili 7 mwaka huu Cairo. Tenga ni mgombea pekee wa nafasi hiyo
kwa Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.
Pia Rais Tenga amezungumzia msimamo wa bara la Afrika uliowekwa
katika Mkutano Mkuu wa CAF uliofanyika mwaka jana jijini Sao Paulo, Brazil kuwa
wanachama wote wa CAF watamuunga mkono Rais wa sasa wa FIFA anayetetea nafasi
yake katika uchaguzi utakaofanyika Mei mwaka huu jijini Zurich, Uswisi.
Vilevile Mkutano Mkuu wa CECAFA uliofanyika
Desemba 2014 jijini Nairobi, Kenya ulipitisha azimio la kumuunga mkono Joseph
Sepp Blatter katika uchaguzi wa FIFA.
Katika mkutano huo, Rais wa TFF, Jamal Malinzi ametoa tamko rasmi
kuwa kwa niaba ya TFF atampigia kura Joseph Sepp Blatter.
No comments:
Post a Comment