Na Hadija Jumanne, Mwananchi
Dar es Salaam. Utafiti mpya umebaini kuwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanaongoza kwa unywaji wa pombe hasa ya viroba, ikiwa ni mara nne zaidi ya wakazi wanaokunywa pombe katika mikoa ya Mwanza na Geita.
Katika utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiri wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kupitia mradi wa Strive ulibaini kuwa idadi kubwa ya wanaokunywa pombe ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24.
Utafiti huo wa NIMR ulilenga kujua ukubwa wa Matumizi ya Pombe kwa vijana katika mikoa ya Kilimanjaro, Mwanza, Geita na Kahama umebaini kuwa mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa unywaji wa pombe kwa vijana wenye umri kutokana na utamaduni uliopo mkoa huo.
Akitoa matokeo ya utafiti huo uliopewa jina la ripoti ya utafiti wa ukubwa wa matumizi ya pombe nchi, Dar es Salaam, Mtafiti wa NIMR Dk Saidi Kapiga alisema hapa nchini matumizi ya pombe ni makubwa na wanaume wanaongoza kwa kunywaji wa pombe kuliko wanawake licha ya kuwa na madhara kwa watumiaji.
“Hapa nchini matumizi ya kiwango cha pombe ni makubwa na wanaume wanaongoza kwa utumiaji wa pombe kwa asilimia 25 hadi 30 ikilinganishwa na wanawake ambao ni asilimia 8 hadi 15 na hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wizara ya afya na ustawi wa jamii miaka miwili iliyopita”alisema Dk Kapiga.
Utafiti wa Mwanza, Geita na Kahama
Alisema utafiti uliofanywa na NIMR katika mikoa ya Mwanza, Geita na Kahama kwa kipindi cha mwaka jana ulibaini wanaume wanaongoza, kwani kati ya watu wazima 1000 tuliowauliza juu ya matumizi ya pombe, asilimia 28.5 ya wanaume na wanawake asilimia 13.
Mtafiti wa Sayansi ya Jamii kutoka kituo cha NIMR mkoani Mwanza, Haika Osaki amesema utafiti waliofanya katika Mkoa wa Kilimanjaro ulihusisha matumizi ya pombe aina ya viroba.
Osaka alisema walishirikisha vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 kutoka katika makundi ya shule, vyuo na vibarua ambapo utafiti ulibaini kuwa vijana wengi wanajiusiha na matumizi ya pombe kali aina ya viroba kutokana na bei ndogo ya bidhaa hiyo.
CREDIT: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment