Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar
Na Miza Othman,
Maelezo-Zanzibar
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinbuzi Mhe.
Ali Mohamed Shein amesema kuanzishwa kwa vikundi vya ushirika (SACCOS) ni njia
moja ya kujiimarisha kiuchumi na kupambana na umasikini Visiwani Zanzibar.
Ameyaeleza hayo katika
hafla ya uzinduzi wa Ushirika wa Jitihada Njema wa Bandari ya Zanzibar huko ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini
Zanzibar.
Amesema uanzishwaji wa vikundi vya ushirika hasa wa vijana na
kinamama, ni njia ya kuendesha maeneo maalumu ya kufanyia shughuli zao za
Biashara ndogondogo pamoja na kuzitambua rasilimali ambazo ziko kwenye sekta zisizo
rasmi vikiwemo vikundi hivyo.
Dr. Shein amesema lengo la Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, ya awamu ya saba ambayo azma yao ni kuviimarisha vikundi
vya ushirika vinavyokwenda sambamba na ilani ya uchaguzi Mkuu ya Chama cha CCM
ya Mwaka 2010 ambalo amelibainisha wakati alipozinduwa Baraza la nne la
Wawakilishi tarehe 11 Novemba 2010
katika hutuba yake ya uzinduzi huo.
Aidha ameeleza kuwa
kufanya hivyo ni kuimarisha Mfuko wa Uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ili kukuza
uwezo wa kutowa mikopo kwa wananchi na kuwawezesha kutumia fursa zilizopo
katika maeneo yao.
Hata hivyo amesema
Serikali itashirikiana nao katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili
ili waweze kupata ufanisi zaidi wa kuendeleza vikundi vyao.
Wakiwasilisha risala
yao wana kikundi cha ushirika wa Jitihada Njema wameliomba Shirika la Bandari
la Zanzibar kuwapatia kiwanja ili waweze kujenga ofisi yao kwa lengo la
kukiendeleza kikundi chao.
Pia wamesema kwamba
lengo la Ushirika wao ni kuwapatia mikopo wananchi, kuutangaza ushirika wao ndani
ya jamii ili kuwatengenezea ajira
vijana, kutatuwa changamoto zinazowakabili wanaushirika hao, kusaidia kujuwa
mbinu mbalimbali za elimu na kuwarahisishia upatikanaji wa Bima ya Afya.
Hata hivyo wamesema
tatizo kubwa kwa sasa linalowakabili katika kikundi cha ushirika wao ni ukosefu wa ofisi yenye eneo la kutosha kwa ajili ya shughuli
zao jambo ambalo linawarejesha nyuma kwa kiasi kikubwa katika utendaji wao kazi.
Ushirika huo
ulianzishwa tarehe 31 Januari, 2004 ikiwa na wanachama 100 na hadi sasa una wanachama
200 na tayari wameshafunga mkataba wa kupatiwa mikopo na Shirika la Bandari.
No comments:
Post a Comment