Viongozi wa mashtaka nchini Ujerumani wanasema kuwa wamepata ushahidi unaosema kwamba rubani wa ndege ya Ujerumani ilioanguka katika milima ya ALPS na kuwaua abiria 150 alikuwa amemficha mwajiri wake kuhusu ugonjwa anaougua.
Maafisa hao pia wamesema kuwa walipata kijikaratasi cha ugonjwa kilichokuwa kimekatwa ambacho kilimtaka rubani huyo kupumzika siku ya kuanguka kwa ndege hiyo.
Hatahivyo hawakupata ujumbe wowote wa rubani huyo kutaka kujitoa uhai wake.
Vyombo vya habari nchini Ujerumani vimeripoti kwamba faili ya rubani Andreas Lubitz mwenye umri wa miaka 27 katika shirika la anga za juu imeonyesha kuwa Andreas alikuwa na matatizo ya akili na alitakiwa kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara.
Ripoti nyengine ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa alilazimika kuchukua likizo ya miezi sita kutoka kwa mafunzo ya urubani kutokana na shinikizo la akili.
Katika hatua nyingine, Polisi nchini Ujerumani wamegundua kile wanachosema kitawasaidia katika kubaini kiini cha rubani msaidizi Andreas Lubitz, kuangusha ndege na kuwauwa abiria wote 150.
Hayo ni baada ya kufanya msako katika nyumba yake.
Polisi hawajatoa taarifa zaidi kuhusiana na kile walichokipata, lakini baadhi ya vitu vyake vikiwemo Kompyuta, vimechukuliwa ili kuchunguzwa.
Huku uchunguzi huo ukiendelea, imebainika kuwa rubani huyo alitatiza kwa muda, mafunzo yake ya urubani mwaka 2008, kutokana na kutibiwa matatizo ya kiakili
Waziri wa maswala ya ndani nchini Ujerumani, Tomas de Maiziere, anasema kuwa, uchunguzi wa kiusalama dhidi ya rubani huyo, haujasema lolote huku, muajiri wake kampuni ya Lufthansa, ikisizitiza kuwa Lubitz alikuwa asilimia mia kuendesha ndege.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment