Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe (aliyevaa jaketi lenye ramani ya Tanzania) akiwa na mamia ya
washariki wa matembezi ya hisani ya kuhamasisha kukomeshwa kwa mauaji ya watu
wenye ualbino nchini. Matembezi hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Imetosha
yalianza katika viwanja vya Biafra na kuishia viwanja vya Leaders Club wilayani
Kinondoni, ambapo vikundi mbalimbali vya mazoezi ya viungo jijini Dar es Salaam
vilishirikishwa pamoja na wageni waalikwa akiwemo Mbunge wa Viti Maalum, Al
Shaimar Kweigyir pamoja na Jaji wa Mahakama Kuu, Hamisa Kalombola. Picha zote Felix Mwagara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe (wanne kulia), Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir
(wanne kushoto), Jaji wa Mahakama Kuu, Hamisa Kalombola (watatu kushoto) pamoja
na Viongozi na Wanaharakati wa Taasisi ya Imetosha inayopambana na kutokomeza
mauaji ya watu wenye ualbino nchini wakiimba wimbo wa Tanzania Nakupenda katika viwanja vya Leaders Club mara baada ya kufanya Matembezi ya Hisani yaliyoanzia
viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo yaliandaliwa
na Taasisi hiyo kwa kuwashirikisha mamia ya washariki kutoka katika vikundi
mbalimbali vya mazoezi ya viungo jijini Dar es Salaam pamoja na wageni waalikwa.
Mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa hotuba yake yenye kulaani mauaji
ya albino nchini mbele ya viongozi na wanaharakati wa Taasisi ya Imetosha inayopambana
na kutokomeza mauaji ya watu wenye ualbino nchini pamoja na mamia ya washiriki wa Matembezi ya Hisani (hawapo pichani). Katika hotuba yake, Chikawe aliwaomba
wananchi washirikiane na serikali kikamilifu katika kuwalinda watu wenye ualbino
ili kusambaratisha mauaji hayo ambayo yanaendelea hasa katika mikoa ya Kanda ya
Ziwa. Hata hivyo, Chikawe alisema Jeshi la Polisi linaendelea kuwakamata
watuhumiwa pamoja na kutoa ulinzi mkali kwa albino, pia alisema Serikali
itashirikiana na Taasisi hiyo ili kuendelea kupinga ukatili huo wanaotendewa
albino. Waziri Chikawe alisema hayo baada ya kushiriki matembezi hayo
yaliyoanzia viwanja vya Biafra na kuishia viwanja vya Leaders Club jijini Dar
es Salaam jana.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar
Kweigyir (watatu kushoto), washiriki wa Matembezi ya Hisani ya kupinga mauaji
ya albino wakilisakata rumba mara baada ya kufanya matembezi hayo yaliyoandaliwa na Viongozi na Wanaharakati wa Taasisi ya Imetosha inayopambana
na kutokomeza mauaji ya watu wenye ualbino nchini. Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), aliyaongoza matembezi hayo yaliyoanzia
viwanja vya Biafra na kuishia viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam jana
na kuwaomba wananchi washirikiane na Serikali kuwalinda watu wenye ualbino ili
kusambaratisha mauaji hayo ambayo yanaendelea nchini.
Balozi wa Taasisi ya Imetosha
ambaye pia ndiye mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Henry Mdimu akitoahotuba yake
fupi kwa mgeni rasmi pamoja na mamia ya washiriki (hawapo pichani) wa matembezi ya hisani ambayo yaliandaliwa na taasisi hiyo ikiwa ni Kampeni Maalum ya
kupinga mauaji ya albino nchini. Kwa mujibu wa Mdimu, taasisi yake inatarajia
kwenda katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kutoa elimu kwa wananchi hao kuhusiana
na imani potofu dhidi ya mauaji ya albino.
Sehemu ya washiriki
wa Matembezi ya Hisani ya kupinga mauaji ya albino nchini wakifanya mazoezi ya
viungo baada ya kufanya matembezi hayo yaliyoandaliwa na Viongozi na
Wanaharakati wa Taasisi ya Imetosha inayopambana na kutokomeza mauaji ya watu
wenye ualbino nchini. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo
pichani), aliyaongoza matembezi hayo yaliyoanzia viwanja vya Biafra na kuishia
viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam na kuwaomba wananchi washirikiane
na Serikali kuwalinda watu wenye ualbino ili kusambaratisha mauaji hayo ambayo yanaendelea nchini.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Imetosha,
Masoud Kipanya (kulia) akielezea jinsi yeye pamoja na Balozi wa Taasisi hiyo,
Henry Mdimu (kushoto) pamoja na viongozi wengine wa taasisi hiyo, walivyopania kuhakikisha wanasambaratisha mauaji ya albino nchini. Taasisi hiyo imefanya matembezi
ya hisani ikiwa ni kampeni maalum ya kupinga mauaji ya albino nchini. Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), aliyaongoza matembezi
hayo yaliyoanzia viwanja vya Biafra na kuishia viwanja vya Leaders Club jijini
Dar es Salaam na kuwaomba wananchi washirikiane na Serikali kuwalinda watu
wenye ualbino ili kusambaratisha mauaji hayo ambayo yanaendelea nchini. Picha zote na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment