Na Abdulla Ali na Rahma
Khamis Maelezo-Zanzibar
Kifafa cha Mimba ni miongoni
mwa mambo matano makuu yanayosababisha vifo vya moja kwa moja vya akina mama
wajawazito Nchini.
Hayo yameelezwa na Naibu
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahamoud Thabit Kombo wakati akijibu swali la
mwakilishi wa nafasi za wanawake Mhe. Shadya Mohammed Suleiman katika ukumbi wa
Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar aliyetaka kujua ni
vipi wizara ya afya Zanzibar imejipanga kukabiliana na tatizo la vifo vya akina
mama wajawazito vinavyotokea wakati wa kujifungua.
Amesema kuwa miongoni
mwa mambo yanayosababisha vifo vya moja kwa moja vya akina mama ni pamoja na Kutokwa
na damu nyingi kabla au baada ya kujifungua (Haemorrage), Shindikizo la damu
wakati wa ujauzito (Hypertensive Disorder During Pregnancy), Uzazi kanadamizi (Obstructed
Labour), Maambukizo kwenye mfumo mzima wa damu (Sepsis) ambavyo hupelekea
kuharibika au utoaji wa mimba usio salama unaopelekea unaopelekea maambukizi
kwenye mfumo mzima wa damu (Septic Abortion).
Amefahamisha kuwa Serikali
kupitia Wizara yake imekuwa ikiwashajihisha sana akina mama kuanza kwenda vituo
vya afya mapema kwa ajili ya kupima ujauzito ambapo mama mjamzito anatakiwa
kuhudhuria kituo cha afya kila baada ya wiki 2 hadi Mwezi 1.
Ametanabahisha kuwa
iwapo akina mama watakwenda vituo vya afya mapema itawapelekea kuvifahamu
viashiario hatari kwa wakati ambavyo vitaweza kushughulikiwa na kutafutiwa
ufumbuzi kwa muda muwafaka kama miongozo ya huduma ya dharura kwa akina mama na
watoto wachanga inavyoeleza.
Hata hivyo Naibu huyo
amewataka akina mama wajawazito kuhudhuria vituo vya afya mapema na kwa
mpangilio maalum unaoshauriwa na wataalamu wa afya kwani kutasaidia kupunguza matatizo
ya vifo kwa akina mama hao wakati na baada ya kujifungua.
Sambamba na hayo amesema
Wizara yake inajitahidi kuongeza wafanyakazi katika vituo vya afya mbalimbali
vilivyopo Nchini hususan Vijijini kwa mujibu wa hali ya kiuchumi
itakavyoruhusu.
No comments:
Post a Comment