Mahakama ya juu nchini India imefutilia mbali kipengee cha sheria kali iliyowapa polisi uwezo wa kuwashtaki watu kutokana na maoni yao kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.
Mahakama ya juu zaidi nchini humo imesema kuwa kipengee hicho cha 66A iliyolenga kudhibiti sekta ya utandawazi ilikuika katiba ya taifa na haswa kipengee cha uhuru wa kujieleza.
Katika miaka ya hivi karibuni ,watu wengi wamejipata matatani kutokana na semi zao na maoni kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter.
Serikali ilikuwa inajitetea kwa kusema kuwa sheria hiyo kali ilikuwa ikilenga kudhibiti visa vya raia kuweka habari za chuki na matusi kwenye mitandao ya kijamii.
Uamuzi huu wa mapema leo ulitolewa na majaji wawili kufuatia ombi la rufaa kutoka kwa wanaharakati wa haki za kibinadamu nchini humo
na mwanafunzi wa sheria katika chuo kikuu kimoja nchini humo ambao walilalamika kuwa sheria hiyo ilikuika uhuru wa kujieleza uliokuwa umelindwa na katiba ya nchi.
"kipenge cha 66A kinakiuka katiba na hivyo ninaamuru kifutiliwe mbali ''shirika la habari la AFP lilimnukuu jaji RF Nariman.
"haki ya kikatiba ya raia wote kufahamishwa inakiukwa kwa sehemu kubwa tu'' aliongezea.
Kulingana na kipengee hicho,66A wahindi walioikashifu serikali idara zake wangelishikwa na kufungwa hata kwa miaka mitatu.
Wanaharakati wanasema kuwa mtu angeweza kufungwa kwa ''kutuma barua ambayo ingezua mjadala mkali na kusababisha usumbufu''
Sheria hiyo ilipingwa vikali na mwanafunzi huyo mwaka wa 2012 baada ya wasichana wawili kukamatwa Mumbai kwa kutoa maoni yao kufuatia mauaji ya mwanasiasa maarufu Bal Thackeray.
Shaheen Dhada alikamatwa kwa kukashifu hatua ya serikali kuimarisha usalama mjini Mumbai punde baada ya kifo chake Thackeray.
Kwa upande wake Renu Srinivasan, alikamatwa kwa ku'like'' ujumbe huo.
Kumekuwa na idadi kubwa ya wanaharakati waliokamatwa kwa kutumia sheriahiyo inayodaiwa kuwa katili.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment