Na Hastin Liumba, Nzega
MWANAMKE mmoja wilayani Nzega mkoani Tabora ameuawa kwa kukatwa katwa mapanga na watu wasio fahamika na kufariki dunia.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Tabora, Juma Bwire, alisema tukio hilo limetokea mwezi March 28 mwaka huu katika kitongoji cha Ngukumo B wilayani Nzega mkoani Hapa.
Alimtaja mwanamke huyo aliyeuawa kuwa ni Madegeleke Uswelu Malangala (55) ambapo alidai watu wasio fahamika majira ya saa mbili usiku walivamia nyumbani kwake kisha kuanza kumshambulia kwa mapanga mpaka kusababisha kifo chake.
Bwile alisema sababu za mauaji hayo ya kikatili ni kutokana na iamani potofu za kishirikina zilizo kithiri baadhi ya maeneo ya mkoa wa Tabora ambazo zimekuwa zikihatarisha maisha ya vikongwe na wanawake ambao hawana hatia.
Alisema kuwa jeshi la polisi mkoani linaendelea na upelelezi wa mauaji hayo ilikubaini walitenda na kushiriki na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano mkubwa kwa polisi ilikuwabaini waliotenda mauaji hayo.
Alisema kwa sasa jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu wanaosababisha kukithiri kwa imani hizo ikiwana kuiomba jamii ibadilike katika kuamini imanai potofu.
Baadhi ya wananchi wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa masharti ya kutokuandikwa majina walisema mwanamke huyo ameuawa kinyama kutokana na majeraha aliyokuwa nayo na kuiomba serikali kuendelea na juhudi za kuwasaka.
Wananchi hao waliwatuhumu baadhi ya waganga wajadi kuendelea kupiga ramli chonganishi ambazo zimekuwa zikiteketeza maisha ya wanawake, watu wenye ulemavu wa ngozi Albino na kusababisha mayatima.
Walisema kuwa serikali inapaswa kutoa mafunzo mbalimbali ikiwa na semina zakukemea mauaji hayo ambayo yamekithiri katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
No comments:
Post a Comment