Vikosi vya MONUSCO
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kupunguza vikosi vyake vya kijeshi vilivyoko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo -DRC, vikosi ambavyo vina askari wengi zaidi ulimwenguni.
Azimio hili limekuja baada ya waziri wa Mambo ya nje wa Jamhuri wa Kidemokrasi ya Congo -DRC- kutoa tamko katika baraza la uslama la umoja wa mataifa mwishoni mwa wiki iliyopita, kwamba nchi hiyo iko tayari kuchukua majukumu ya kuhakikisha usalama wake, kutoka katika vikosi vya Umoja wa Mataifa.
Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa mataifa kinachojulikana kama MONUSCO kina zaidi ya wanajeshi 19,000, na kuongoza kuwa na wanajeshi wengi duniani, katika wiki zijazo kitapoteza karibu asilimia 10 ya askari wake hao.
Katika ombi lake hilo kwa baraza la usalama Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo alitaka pia kuharakishwa kupunguzwa kwa jeshi hilo.
Hata hivyo Umoja wa Mataifa na makundi mbalimbali ya kiraia hayakubaliani na hoja hiyo. Yanasema kuwa kikosi hicho kinapaswa kuimarisha uwepo wake nchini humo na upunguzwaji wowote lazima ufanyike polepole.
Kiongozi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo amesema mengi yanahitajika kufanyika kupunguza kitisho vya vikundi vya wapiganaji dhidi ya raia na kwamba kuijitoa kokote kwa jeshi hilo lazima kufanyike taratibu.
Nayo makundi mbalimbali ya kijamii yamekitaka kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa kuongeza wanajeshi wake Jamguri ya Kidemokrasi ya Congo katika kipindi ambacho uchaguzi wa Rais nchini humo unafanyika mwaka ujao.
Makundi ya haki za binadamu yanataka wanajeshi zaidi wa kulinda amani waongezwe nchini humo katika kipindi cha kuelekea uchaguzi, ili kuwalinda raia.
Zaidi ya makundi ya wapiganaji yapatayo 30 bado yanaendelea na shughuli zake mashariki mwa nchi hiyo, huku mamia kwa maelfu ya watu wakilazimika wakilazimika kuyakimbia makaazi yao kwa zaidi ya muongo mmoja.
Wachunguzi wengi wa mambo wameelezea pia wasiwasi wao kwamba serikali labda inajaribu kuiondoa jumuia ya kimataifa katika mchakato wa uchaguzi.
Inakadiriwa kuwa watu 42 waliuawa Januari mwaka huu katika maandamano ya kupinga Rais kuongezewa muda madarakani.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment