- Ampongeza Mbunge Lekule kwa uamuzi wake wa kutogombea tena
- Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha alia na watendaji wa serikali,asema ndio wanakiumiza chama
- Nape awapongeza wana CCM wilaya ya Longido kwa mshikamano na kuipa ushindi CCM kwenye Chaguzi
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kumchoma ng'ombe chanjo
kwenye mradi wa ufugaji wa madume bora katika kijiji cha Ketumbeine.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Longido Ndugu Michael Lekule Laizer mara baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Engikareti mpakani mwa wilaya ya Arumeru na Longido.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza wimbo maalum
kutoka kwa wenyeji waliokuja kumpokea wa kijiji cha Engikareti.
Loishiro Yaseya Katibu kata ya Engikareti wilaya ya Longido akisoma
risala mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo
walimuelezea tatizo kubwa ni ugomvi wa mipaka na wilaya ya Arumeru.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha
Engikareti waliokuja kumpokea mpakani mwa wilaya ya Longido na Arumeru.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa vazi la kimila la
heshima na wananchi wa Kijiji cha Engikareti wilaya Longido.
Mkuu
wa Wilaya ya Longido Ndugu Ernest Kahindi akiwasalimia wananchi wa
kijiji cha Engikareti wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza wimbo wa mapokezi
alipowasili kwenye kijiji cha Longido kata ya Longido ambapo aliweka
jiwe la msingi katika jengo la hoteli ya kisasa ya mfugaji Ndugu Kitasho
Simel Nakutamba.
Mzee
Kitasho Simel Nakutamba akimpa mkono Katibu Mkuu wa CCM ndugu
Abdulrahman Kinana mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika hoteli
yake ya hapo Longido
Jengo la kisasa linalojengwa kwa ajili ya Hotel na mfugaji Kitasho Simel Nakutamba
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na vijana wa kimasai
alipowasili kwenye kituo cha mafunzo Learning In Longido .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi kwenye majengo ya kituo cha mafunzo cha Learning In Longido.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mapokezi ya aina yake
alipowasili kwenye kijiji cha Ketumbeine ambapo alitembelea mradi wa
ufugaji wa ng'ombe madume bora ya mbegu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiandaa sindano ya chanjo tayari kwa kumchoma ng'ombe.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwenye kijiji cha
Ketumbeine mara baada ya kushiriki kuchoma chanjo za ng'ombe.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya
ufunguzi wa jengo la hoteli katika kijiji cha Kitumbeine,kulia ni
mmiliki wa hoteli hiyo Ndugu Halifa Juma.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wa kijiji
cha Lesingeita ambapo alishiriki ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Afya.
Bendera
ya Chama Cha Mapinduzi ikipepea kwa masaa 24 kwenye kijiji cha
Lesingeita karibu na mradi wa wananchi wa kujenga nyumba za watumishi wa
kituo afya.
Katibu wa Kikundi cha akina mama cha Msanja Flora Kaaya akisoma risala kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Kikundi hicho kinajishughulisha na ufugaji wa mbuzi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua bendera tayari
kuipandisha kwenye shina la wakereketwa wa Madereva wa Noah na Hiace
pamoja na wafanya biashara ndogo ndogo Namanga
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Eworendeke
ambapo alimpongeza mbunge wa jimbo la Longido kwa uamuzi wake wa
kutogombea uchaguzi ujao na kusema wanasiasa wengi wanajua kuingia
kwenye siasa lakini wakisahingia hawajui wakati gani wa kutoka.
Wananchi wakifuatilia hotuba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa
kijiji cha Eworendeke ambapo alisema ni makosa makubwa kwa wanaowania
nafasi za kugombea kupita pita kabla ya wakati rasmi kwani kunapunguza
ufanisi wa viongozi waliopo madarakani.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Eworendeke
ambapo alitoa salaam za shukrani kwa CCM wilaya ya Longido kwa kuipa
ushindi mzuri wakati wa uchaguzi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi na bendera za
laiyekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Longido ambaye amejiunga
na CCM kwenye mkutano uliofanyika Eworendeke.
Wananchi wakisikiliza hotuba kwa makini.
Mbunge wa Jimbo la Longido Mh.Michael
Lekule Laizer akihutubia wananchi wa Eworendeke ambapo aliwaambia
wananchi hao kuwa hatogombea kwenye uchaguzi ujao wa Oktoba 2015.
No comments:
Post a Comment