Rais Macky Sall wa Senegal ameomba kupunguza muhula wake kwa miaka miwili
Rais wa Senegal Macky Sall
amependekeza kura ya maamuzi kuhusu kupunguzwa kwa muhula wake kwa miaka
miwili,hatua ambayo ni kinyume na ile ya viongozi wengi wa Afrika ambao
wanataka kusalia madarakani maisha.
Kulingana na gazeti la the Guardian nchini Uingereza,hatua hiyo inajiri wakati ambapo mataifa ya Benin,Rwanda,Burundi na Congo Brazzaville yanataka kubadilisha sheria ili viongozi wake waendelea kuhudumu kwa muhula wa tatu.
''Nilichaguliwa kwa miaka saba,lakini mwaka ujao nitapendekeza kufanyika kwa kura ya maamuzi ili kupunguza muhula wangu'',aliuambia mkutano na vyombo vya habari mjini Dakar.
Msimamo huo utasababisha kuangaziwa kwa katiba hususan kuhusu mamlaka na baadaye kuhusu vipengee vyengine vya kuimarisha demokrasia,alisema akiongozea kwamba angependelea kura hiyo kufanyika mwezi Mei mwaka ujao.
''Je,ushawahi kuona rais akipunguza muhula wake wa kutawala?'',basi mimi nitafanya ,Sall aliuambia mkutano huo akitoa ahadi hiyo ambayo ni baadhi ya ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2012.
CREDIT: BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment